Zuchu ajibu madai ya kugura lebo ya WCB

" aahh huyo si chini ya 10 billion si unaona manamba yake huko mjini Youtube baba,"Alisema Diamond.

Muhtasari
  • Zuchu ajibu madai ya kugura lebo ya WCB

Msanii maarufu kutoka Tanzania Zuchu, kupitia kwenye mahojiano na Wasafi TV amesema kwamba hana shida kulipa bilioni iwapo anataka kugura lebo ya WCB inayomilikiwa na staa wa bongo Diamond Platnumz.

Hii ni baada ya staa wa bongo Diamond kusema kwamba angelipa bilioni ya mapesa iwapo msanii huyo angetaka kutoka kwenye lebo yake.

Diamond alikuwa anamjibu shabiki aliyemuuliza Zuchu angelipa pesa ngapi.

" aahh huyo si chini ya 10 billion si unaona manamba yake huko mjini Youtube baba,"Alisema Diamond.

Huku Zuchu akijibu matamshi ya bosi wake alisema;

"Msanii anapoamua kubaki au kuondoka kwenye lebo naamini kila mkataba una makubaliano yanayopendelea pande zote mbili,Ulikaa na kukubaliana, ikiwa ni shimo uliloingia ulichimba hela mwenyewe."

Aliongeza kuwa;

"Ikiwa kuna mambo ulitaka yabadilishwe ulikuwa na nafasi ya kufanya hivyo mwenyewe.Kila kitu kinajadiliwa,Wasanii walikuwa wanaondoka WCB hata kabla sijajiunga, kama ingetegemea mambo mengine ningesaini mkataba."