Nyamira: Miaka 10 ya ugatuzi bila uwanja, shule itafungwa ili kutumia uwanja kuapisha gavana

Baadhi wanasema kaunti hiyo ni miongoni mwa kaunti zisizo na cha kujivunia katika miaka 10 iliyopita ya ugatuzi

Muhtasari

• Agosti 25 katika uwanja wa shule ya msingi ya Nyamira kuanzia saa 9 asubuhi ndio itakuwa siku ya kuapishwa kwa gavana na naibu wake.

• Hii inamaanisha kwamba wanafunzi katika shule hiyo hawataenda shule Alhamisi Agosti 25 ili kupisha shughuli hiyo ya kiserikali.

Gavana mteule wa Kaunti ya Nyamira
Amos Nyaribo Gavana mteule wa Kaunti ya Nyamira
Image: MAKTABA

Kaunti ya Nyamira ni moja kati ya kaunti ndogo sana nchiki Kenya na inatajwa kuwa moja ya kaunti ambazo hazijapata manufaa mengi tangu kuanzishwa kwa serikali za ugatuzi kutokana na kile baadhi ya wachanganuzi wa siasa na uchumi wa kimaeneo wanasema ni viongozi wasiowajibika.

Baada ya miaka kumi ya serikali ya kaunti hiyo, wengi kutoka eneo hilo wanasema kwamab hakuna muundo mbinu au miundo msingi ya maana ambayo uongozi unaweza ukasema umewekea wenyeji ili kuonesha matunda ya ugatuzi.

Mjadala kuhusu matumizi mabaya ya fedha za ugatuzi zinazonuiwa kufaidi kaunti hiyo kimaendeleo umekuwa ukizungumziwa sana katika vyombo vya habari vinavyopeperusha matangazo yao kwa lugha ya Abagusii na pia katika mitandao ya kijamii.

Sasa jana mjadala huo uliibuka tena baada ya mtanagzaji kutoka kituo kimoja cha redio ya Abagusii kupakia kwenye mitandao barua iliyokuwa imeandikwa na katibu wa kaunti hiyo pamoja na mwenyekiti wa kaamti ya kuwaapisha gavana mteule na naibu wake.

Barua hiyo ilikuwa inawaalika wawili hao kuhudhuria mkutano wa kuwaapisha huku pia ikiwaalika viongozi wengine kama seneta, mwakilishi wa kike, wajumbe kutoka maeneo manne ya bunge miongoni mwa wengine.

Kilichoibua mjadala huu ni kwamba barua hiyo inasema sehemu ya sherehe ya kuapishwa kwa gavana na naibu wake itakuwa katika uwanja wa shule ya msingi ya Nyamira, jambo ambalo wengi walisema kwamab hata baada ya miaka kumi ya ugatuzi, Nyamira haijajenga hata uwanja mmoja wa kufanyika kwa sherehe kaam hizo na kusikitika kwamab siku hiyo shule italazimika kufungwa ili kutoa nafasi kwa gavana na naibu wake kulishwa kiapo cha kuhudumu kwa miaka 5 ijayo.

“Hongera kwa kuchaguliwa kwenu. Kamati ya kuapisha gavana na naibu wake ingependa kuwaalika kwa siku ya kuapishwa kwa gavana mteule Amos Nyaribo na naibu wake James Gesami mnamo Agosti 25 katika uwanja wa shule ya msingi ya Nyamira kuanzia saa 9 asubuhi,” sehemu ya barua hiyo inasoma.

Nyamira
Nyamira

Hilo la kuandaa sherehe ya kiserikali katika uwanja wa shule na ni siku ya kawaida ya watoto kuhudhuria masomo liliwapata wengi ambapo walionesha mfadhaiko wao na uongozi wa miaka 10 iliyopita wa kaunti hiyo.

“Ombeeni kaunti ya Nyamira kwa jumla, watalazimika kufunga shule ili kuwaapisha gavana na naibu wake. Hakuna hata uwanja mmoja baada ya miaka 10,” mmoja kwa mfadhaiko mkubwa aliandika.