Lilian Ng'ang'a afunguka kwa nini hakupata mtoto na Alfred Mutua

Lillian na Mutua walikuwa pamoja kwa miaka minane

Muhtasari

•Katika mahojiano maalum na mwandishi Elizabeth Ngigi, Lillian alisema yuko kwenye ndoa yenye furaha sana na Juliani.

•Mama huyo wa mtoto mmoja mwenye umri wa miaka 37 alisema kuwa mama ni tukio la ajabu.

Image: INSTAGRAM// LILIAN NG'ANG'A

Ni takriban mwaka mmoja sasa tangu Lilian Ng’ang’a na mumewe Juliani kutangaza mahusiano yao ya kimapenzi. Lilian alithibitisha mahusiano yake na Juliani wiki chache tu baada ya kukatisha ndoa yake na aliyekuwa mwenzi wake, gavana wa zamani Alfred Mutua.

Juliani katika mahojiano ya awali alisema kuwa hakupanga kujitosa kwenye mahusiano na Lillian, lakini mambo yalizidi kasi baada ya Lillian kuchukua namba yake.

Mwaka mmoja baadaye, wawili hao ni wazazi wa mtoto wa kiume anayeitwa Utheri (mwanga).

Katika mahojiano maalum na mwandishi Elizabeth Ngigi, Lillian alisema yuko kwenye ndoa yenye furaha sana na Juliani.

"Mwaka wangu mmoja na Juliani umekuwa rahisi sana na hivyo ndivyo mapenzi yanavyopaswa kuwa. Inapaswa kuwa rahisi kama kupumua. Naipenda kwa sababu, huyu ni mtu ambaye ananitakia mema zaidi ya kila kitu," alisema.

Wakati wa mahojiano, mwandishi alimuuliza Lillian ikiwa alipanga kupata mtoto wake. Alieleza;

"Kila kitu hutokea kwa sababu na ni nadra sana kukaa chini na kukubaliana kwamba tungependa kupata watoto Julai," alisema.

"Lakini sasa kwa kuwa mtoto yuko hapa, singembadilisha kwa chochote. Ni jambo bora zaidi kuwahi kutokea katika maisha yangu. Mimi ndiye mama mwenye furaha zaidi duniani."

Lillian na Mutua walikuwa pamoja kwa miaka minane. Alipoulizwa ikiwa hakutaka kupata mtoto wakati huo, Lillian alifichua;

"Hakuna mtu ambaye huwa tayari kuwa na mtoto. Mimi niko wazi kwa ulimwengu na kila kitu kinachoweza kutokea. Ninachukua kila kitu kinachokuja kwenye maisha yangu kama yalivyo na inaweza kuonekana kama ni nje ya kawaida, lakini kila kitu hutimiza kusudi. Ninashukuru kwa kila jambo."

Mke huyo wa sasa wa Juliani amejibu kwa nini hakupata mtoto na gavana wa zamani wa Machakos Alfred Mutua.
Gavana wa zamani wa Machakos Alfred Mutua na aliyekuwa mpenzi wake Lilian Ng'ang'a Mke huyo wa sasa wa Juliani amejibu kwa nini hakupata mtoto na gavana wa zamani wa Machakos Alfred Mutua.
Image: INSTAGRAM//GOVERNOR ALFRED MUTUA

Mama huyo wa mtoto mmoja mwenye umri wa miaka 37 alisema kuwa mama ni tukio la ajabu.

"Kwa sasa, siwezi kufikiria kuwa na watoto wengine lakini uzazi umeleta upendo tofauti na majukumu zaidi na sasa nataka kufanya kazi kwa bidii zaidi kwa ajili yao na kujifunza mengi."

Lillian alimtaja Juliani kuwa baba mzuri kwa mtoto wao.

"Anasaidia sana, kubadilisha mtoto, kucheza nao na ninafurahi kumuona akiwa baba," alisema.

(Utafsiri: Samuel Maina)