Hisia mseto baada ya Juliani ‘kuomba’ msaada kulea mwanawe Lilian

Hisia mseto baada ya Juliani ‘kuomba’ msaada kulea mwanawe Lilian

"Chochote unaweza kitasaidia. Ni wenu, ni Rapa/mjasiriamali anayeteseka," Juliani aliadika.

Muhtasari

• Juliani alidai kuwa amefilisika na kuwaomba Wakenya kumchangia pesa za kununua diapers za mwanawe mdogo kupitia Mpesa.

• Amewataka wanamitandao kuuchukulia ujumbe huo kwa dharau.

Juliani katika matembezi na mwanawe
Image: INSTAGRAM// JULIANI

Mwanamuziki wa nyimbo za kufoka Julius Owino almaarufu Juliani amewasha moto kwenye Twitter baada ya kuchapisha ujumbe wa utani akiomba msaada wa malezi ya mwanawe na Bi Lilian Nganga.

Katika chapisho lake la utani Jumatano asubuhi, Juliani alidai kuwa amefilisika na kuwaomba Wakenya kumchangia pesa za kununua nepi  za mwanawe mdogo kupitia Mpesa. Alijitambulisha kama rapa  na mjasiriamali anayeteseka.

"Wase! Nikubaya niko BROKE! mtoi anahitaji pampers.. Tafadhali tumeni mpesa. Lipa na M-PESA 784577, Akaunti- Juliani," aliandika.

"Chochote unaweza kitasaidia. Ni wenu, ni Rapa/mjasiriamali anayeteseka,"

Ujumbe huo wa utani wa rapa huyo ulifuatia uvumi na habari nyingi za uwongo kuhusu uwezo wake wa kifedha ambazo zimekuwa zikichapishwa kwenye mitandao ya kijamii katika siku za hivi majuzi. 

Amewataka wanamitandao kuuchukulia ujumbe huo kwa dharau kama vile jumbe zingine zinazomhusu ambazo zimesambazwa mitandaoni siku za nyuma.

"Msiwahi kuamini kilicho mitandaoni," alisema.

Mwimbaji huyo alilazimika kujibu baada ya habari za uwongo kusambazwa zikidaiwa kuwa yeye na mkewe wamefilisika.

Baadhi ya ripoti zilidai kuwa msanii  huyo tayari  amekwenda mahakamani ili kumshurutisha gavana wa zamani wa Machakos  Alfred Mutua kugharamia malezi ya mwanawe.

Wanamitandao wengi pia wamekuwa wakimtania Lilian kwa kutengana na Mutua kisha kujitosa kwenye ndoa na Juliani.

Chapisho la Juliani limealika hisia mseto kutoka kwa wanamitandao huku baadhi yao wakianguka kwenye mtego na kuamini ujumbe wa Juliani kwamba amefilisika huku wengine waking'amua kuwa alikuwa tu anawatania.

Hizi hapa baadhi ya hisia za wanamitandao:-

Bevalyne Kwamboka: Kuja upeel waru nikulipe basi.

Tall Hobbit: Na Wakenya wanatuma.

Red Bull Report: Napenda utani huu.

Afya Centre Crew: Unaweza kusimamia Afya Center?

Muraya Wa Kitale: Uko serious bro? Kwani huyo mwanamke wa Mutua alikuja bila kitu?

Irungu Macharia: Mtu amedukua akaunti ya Juliani. @bonifacemwangi mwangalie ndugu yako.