"Ni mapambano!" Akothee afichua kwa nini bado hajamtambulisha mpenziwe kwa mamake

Mwimbaji huyo ameeleza hofu yake kubwa ya kumtambulisha mpenziwe kwa mamake.

Muhtasari

• Mama huyo wa watoto watano amedai kuwa haijawahi kuwa rahisi kwake kumwendea mzazi huyo wake.

•Kwa jinsi ilivyo ngumu kumwendea mamake, Akothee amekuwa akitumia usaidizi wa mjomba wake kumfikia.

Mwimbaji Akothee na mpenzi wake Bw Schweizer
Image: INSTAGRAM// AKOTHEE

Mwimbaji Esther Akoth almaarufu Akothee amefichua kwamba huwa anahofia kuwatambulisha wapenzi wake wapya kwa mamake.

Katika ukurasa wake wa Instagram, mama huyo wa watoto watano amedai kuwa haijawahi kuwa rahisi kumwendea mzazi huyo wake.

Amefichua kuwa amewahi kutambulisha wapenzi wake wawili pekee kwa mamake kwani huwa hapendelei watu kuruka kutoka mahusiano moja hadi mengine. Kufuatia hilo, ameeleza hofu yake kubwa ya kumtambulisha mpenziwe mpya.

"Siku zote nimekuwa nikiona ni vigumu sana kutambulisha mchumba. Nimewatambulisha wanaume 2 tu rasmi kwa Mama yangu Hiyo ni ndoa yangu ya kwanza, na Wuon Oyoo, hii itakuwa ya 3. Na ni mapambano," alisema.

Mwimbaji huyo ametoa ombi kwa mzazi huyo wake kulegeza kamba ili kufanya iwe rahisi kwake kumtambulisha mpenziwe.

"Mama yangu huwa hamtambui mpenzi wako, atakupuuza na hata hata hatakusalimia kwa mkono, msichana huyo anaweza kukugeukia haraka. Mwambieni alegeze kamba, hii bale Iko tu sawa," alisema.

Kwa jinsi ilivyo ngumu kwake kumwendea mamake, Akothee amekuwa akitumia usaidizi wa mjomba wake kumfikia.

Amefichua kuwa kuna urafiki mkubwa kati yake na mjomba huyo na hata huwa anashiriki siri zake zote naye.

"Mjomba wangu ananipenda jinsi tu nilivyo, atakuwa wa kwanza kumwambia siri zangu na kumtuma aende kumwambia dada yake Mhe Kokeyo kuwa nimekutana na mtu," alisema mwimbaji huyo.

Ufichuzi huu unajiri huku mwimbaji huyo akionekana kuendelea kuzama ndani kabisa kwenye huba na mpenziwe mzungu.

Mwezi uliopita alimtambulisha Bw Schweizer kama mpenzi wake mpya, miezi michache baada ya kutengana na Nelly Oaks.