•Mwanadada huyo alidokeza kwamba anatarajia mtoto wake mwezi Machi mwaka kesho.
Kupata ujauzito baada ya muda mrefu wa kujaribu bila mafanikio ni suala ambalo linapokelewa kwa furaha kubwa na wanawake, lakini pia na watu wanaowazunguka na wanaojua umuhimu wa kupata mtoto.
Ndivyo hali ilivyokuwa kwa wazazi wa mwanadada mmoja aliyepakia video kwenye Tiktok yake akionesha jinsi wazazi wake walijawa na furaha na kububujikwa na machozi ya furaha baada ya kuwapa taarifa za kupata ujauzito hatimaye.
Katika klipu hiyo, mwanadada huyo anaonekana akiwapasulia mbarika wazazi wake wazee ambao baada ya kupokea taarifa hizo wanaruka kwa furaha na machozi.
“Nilipowaambia wazazi wangu kwangu hatimaye nimepata ujauzito baada ya kunibembeleza kupata mtoto kwa muda mrefu. Majibu ya wazazi wangu kwa Mtoto Nuñez 🤰🏽❤️ 😂 Nilicheka na kulia na huyu. Majibu ya baba zangu hayana thamani ya kulinganishwa nayo😂 #Tangazo la Mimba #MtotoYuaja #March2023” Mwanadada huyo aliifuatisha video hiyo kwa maneno hayo.
Mwanadada huyo aliwafanyia wanadada wake kama kuwastukiza na kuweka ujumbe huo ndani ya kifurushi na kuwataka wazazi wake wafungue waone kilichokuwa ndani.
Mama yake anaonekana akimuuliza kwa umakini kama ni bangi, jambo ambalo mwanadada anakataa na badala yake kumtaka kuendelea kupekua ndani ili kujionea mwenyewe.
Mama yake baada ya kuona nguo za mtoto mchanga zilizokuwa zikiashiria binti yake ni mjamzito, anaruka kwa kutoamini kabisa na kuanza kutokwa na machozi ya furaha.
Baba mtu naye anaonekana macho yamemtoka bima kabisa na anasikika akisema kwa kuradidi, “tangu lini”
Kwenye upande wa kutoa maoni, mwanadada huyo aliwashukuru mashabiki wake kwa kumtakia heri njema katika safari ya ujauzito wake. Alisema huo ndio ujauzito wake wa pili na mtoto wake wa kwanza ana miaka 14.