Jimal ajipata pabaya baada ya kuwashauri wanamitandao

Muhtasari
  • Kwenye chapisho hilo, mama wa mtoto mmoja ambaye alikashifiwa anadai kuwa wamechumbiana kwani alifichua kuwa walikuwa na sherehe ya kutambulishwa tu
Mfanyabiashara Jimal Rohosafi
Mfanyabiashara Jimal Rohosafi
Image: Instagram//JimalRohosafi

Mfanyibiashara Jimal Roho Safi ameshiriki chapisho la ushauri kwenye ukurasa wake wa instagram, akiwashauri wanamitandao jinsi ya kuishi.

Ushauri wake Jimal haukumwendea vyema kwani asilimia kubwa ya mashabiki walimkejeli.

Hii ni baada ya aliyekuwa mpenzi wake mwanasosholaiti Amber Ray, kushiriki ujumbe kuhusu kutambulishwa kwake kwa wazazi wa mpenzi wake Rapudo.

Kwenye chapisho hilo, mama wa mtoto mmoja ambaye alikashifiwa anadai kuwa wamechumbiana kwani alifichua kuwa walikuwa na sherehe ya kutambulishwa tu.

Naam, baada tu ya Amber kufichua hili kwa umma Jimal  aliendelea na kuchapisha ujumbe wenye utata ambapo alizungumza kuhusu watu kutokuwa na bahati ya mapenzi.

"Ikiwa huna bahati na upendo, fuata pesa.Usiwe mtu wa kushindwa kwa pande zote mbili", ilisoma chapisho la Jimal."

Wafuasi mitandaoni hawakusita kuguswa na chapisho la Jimal. Wengi wa wanamitandao walimwambia Jimal kwamba sasa amekuwa akiwapa watu ushauri baada ya mkewe kukataa kumrudia na mpenzi wake wa zamani pia kuendelea na maisha.

electorsharon: I wish you would reconcile with your wife and be genuine

liliangerthony: πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚Motivational speaker.... Bibi alienda, side hen ameolewa pia. Saa utadu?

mghoi1963: Yani alikuharibia afu sasa ndio yy ndio akaenda officially aki lyf ww πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

mchemunda_hadija: Go and reconcile with your wife big bro..sasa ulimfanya madharau,tena bado unamuonyesha wangari