"Nakupenda!" Guardian Angel amsherehekea binti ya mkewe Esther Musila, Gilda Naibei

"Umebarikiwa kupita kiasi. Kheri ya siku ya kuzaliwa G ❤️ Nakupenda. Mungu akubariki kwa ajili yetu" aliandika.

Muhtasari

•Gilda ambaye ni binti ya Esther Musila kutoka kwa ndoa yake ya awali anasherehekea kutimiza miaka 29 duniani.

•Musila alikiri kujivunia mafanikio ya binti yake na akamtia moyo aendelee kupambana maishani  huku akimuahidi sapoti yake.

Guardian Angel na bintiye wa Kambo Gilda
Image: INSTAGRAM// GUARDIAN ANGEL

Leo hii, Januari 21, Bintiye Esther Musila, Gilda Naibei anaadhimisha siku ya kuzaliwa.

Gilda ambaye ni binti ya Esther Musila kutoka kwa ndoa yake ya awali anasherehekea kutimiza miaka 29 duniani.

Bi Musila na mume wake wa sasa Peter Omwaka almaarufu Guardian Angel wamemsherehekea kipusa huyo anapopiga hatua nyingine maishani.

"Umebarikiwa kupita kiasi. Kheri ya siku ya kuzaliwa G ❤️ Nakupenda. Mungu akubariki kwa ajili yetu" Guardian Angel alimwandikia Gilda kwenye Instagram.

Kwa upande wake, Bi Musila alimsherehekea bintiye na akaonyesha kujivunia maendeleo yake  tangu kuzaliwa hadi mahali alikofikia.

Alimtakia furaha Gilda anapopiga hatua nyingine maishani na akamshauri kwamba kila wakati ajivunie kuwa yeye.

"Nakutakia furaha, amani, upendo na kicheko. Nakuombea kwa Mwenyezi Mungu aendelee kukuongoza na kukulinda siku zote za maisha yako. Ufuate hamu ya moyo wako na ukabiliane na changamoto za maisha zisizoepukika kwa udadisi, sio woga. Huenda nisiweze kukubeba tena mikononi mwangu, lakini nitakubeba moyoni mwangu kila wakati. Nitajaribu kuheshimu kuwa wewe ni mwanamke mzima sasa lakini utakuwa msichana wangu mdogo kila wakati," Bi Musila alimwandikia bintiye.

Musila alikiri kujivunia mafanikio ya binti yake na akamtia moyo aendelee kupambana maishani  huku akimuahidi sapoti yake.

"Kheri ya siku ya kuzaliwa kwako, mama anakutakia baraka za Mungu, afya njema na marejeo mengi yenye furaha. Heri ya siku ya kuzaliwa kwa Maua wetu. Nakupenda 🎉🎊🥂🥂🥂 Tunakupenda Gilda," aliandika.

Gilda ndiye binti pekee wa Miss Musila ambaye ana wana wengine wawili, Jama na Kim kutoka kwa ndoa yake ya awali.

Alifunga pingu za maisha na Guardian Angel mapema mwaka jana lakini bado hawapata mtoto yeyote pamoja.