Watu mashuhuri waliofunga ndoa mwaka wa 2022

Harusi ya Guardian na Esther iliwavutia watu wengi kwa sababu ya tofauti zao za umri.

Muhtasari

•Baadhi ya watu mashuhuri walichagua kutangaza harusi yao huku wengine wakishirika nyakati hizo za furaha faraghani.

Image: INSTAGRAM// ESTHER MUSILA

2022 umekuwa mwaka wa kipekee uliojaa misukosuko mingi. Wakenya wamekuwa na sababu za kutabasamu na pia kumekuwa na nyakati za huzuni.

Mwaka huu unapoelekea kukamilika, tunaangalia nyuma baadhi ya harusi za kupendeza zaidi za watu mashuhuri zilizofanyika.

Baadhi ya watu mashuhuri walichagua kutangaza harusi yao huku wengine wakishirika nyakati hizo za furaha faraghani.

Hapa kuna orodha ya harusi za watu mashuhuri ambazo ziligonga vichwa vya habari mwaka wa 2022:

GUARDIAN ANGEL NA ESTHER MUSILA

Mwimbaji wa nyimbo za Injili Guardian Angel na mke wake Esther Musila walifunga pingu za maiosha katika harusi ya faragha mnamo Januari 4, 2022.

Wenzi hao walifunga ndoa katika harusi ndogo iliyofanyiwa kwenye bustani mnamo siku ya kuzaliwa ya Guardian Angel, alipofikisha umri wa miaka 33.

Walialika wageni 20 tu kwenye harusi yao, watu wa karibu tu ambao walisimama nao tangu waanze kuchumbiana.

"Hatukutaka kila mtu. Orodha yetu ya wageni ilikuwa watu 20. Wengine walikuwa watoa huduma na watu kutoka kanisani, ambao walifanya idadi kuwa 50.

Harusi ya Guardian na Esther iliwavutia watu wengi kwa sababu ya tofauti zao za umri.

Wakati wa harusi yao, mwimbaji huyo wa nyimbo za injili alikuwa na umri wa miaka 33 huku mkewe akiwa na miaka 52.

Esther alisema hakuwahi kufikiria kwamba angempata mtu maalum kama Guardian Angel katika ulimwengu huu.

"Kupata mtu maalum kama wewe kati ya watu wote ulimwenguni ni jambo ambalo sikuwahi kufikiria. Wacha tufanye maisha haya pamoja. Bw & Bi Omwaka," aliandika.

NICK RUTO NA EVELYN CHEMUTAI

Nick Ruto afunga ndoa na kipenzi chake Evylyn Chemutai
Nick Ruto afunga ndoa na kipenzi chake Evylyn Chemutai
Image: HISANI

Mwanawe Rais William Ruto, Nick Ruto alimuoa Evelyn Chemutai katika harusi ya kibinafsi ya kitamaduni katika Windy Ridge, Karen, Nairobi mnamo Januari 15, 2022.

Sherehe hiyo iliwashangaza Wakenya wengi kwani Nick hakuwa amedokeza maisha yake ya uchumba hapo awali.

Chemutai alivalia mavazi ya rangi ya kahawia na alikuwa na nywele zake za asili, huku Nick akiwa amevalia suti nyeupe na kofia ya yenye mguso wa maandishi ya Kiafrika.

Baada ya hafla hiyo, Nick aliandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, "Tulikutana na familia zetu kama utamaduni ulivyodai. Alisema NDIYO, nikasema NDIYO, WAlisema NDIYO, tukasema NDIYO."

Aliongeza, "Shukrani maalum kwa usaidizi wenu na maombi. Evelyne na Nick."

JULIANI NA LILIAN NG'ANG'A

Rapa Julius Owino, almaarufu Juliani, na Lilian Ng'ang'a walifunga ndoa katika hafla ya harusi iliyofanyika Februari 1., 2022.

Hafla hiyo ya chinichini ilihudhuriwa na wageni wasiopungua 50 ambao hawakuruhusiwa kupiga picha za harusi.

Harusi ilifanyika katika bustani ya Paradise katika kaunti ya Kiambu na baadae karamu ikafanyika katika Kentwood Suites, eneo la Runda.

Licha ya kukataza upigaji picha, picha moja ya harusi hiyo iliishia mtandaoni.

Lillian alikuwa amevalia gauni la harusi la waridi, na Juliani alikuwa na shati nyeupe, koti nyeusi na suruali ya rangi nyeusi na viatu vyeupe.

Juliani alikuwa na wasimamizi watatu, wakati Lillian alikuwa na wasimamizi wawili ambao walivaa gauni za lavender begani.

Juliani na mke wake Lilian Nganga
Juliani na mke wake Lilian Nganga
Image: HISANI

Rangi za mandhari ya harusi zilikuwa nyeupe na nyeusi. Chini ya wageni 50 walialikwa.

Alisema kuwa harusi yake ilikuwa rahisi, ambayo ilifanya iwe harusi ya kupendeza.

Alisema picha iliyosambaa mtandaoni ilitoka kwa baadhi ya watu waliokuwa wameenda kujivinjari kwenye ukumbi wa harusi yake. Alitamani watu waheshimu faragha yao.

"Hiyo ilikuwa mbaya. Harusi ni ya faragha. Kwa mtu yeyote kuona hitaji la kusambaza, haikuwa sawa. Lakini kila kitu hutokea kwa sababu," alisema.

AKISA WANDERA NA CHARLES

Mtangazaji wa BBC Akisa Wandera alifunga ndoa na mpenziwe Charles katika harusi ya kitamaduni mnamo Machi 12, 2022.

Harusi hiyo ndogo ilifanyika nyumbani kwake Mundika, kaunti ya Busia, na kuhudhuriwa na familia yake na marafiki wa karibu.

NGINA KENYATTA NA ALEX MWAI

Samuel Mwai na Ngina Kenyatta
Image: KWA HISANI

Binti wa rais wa zamani Uhuru Kenyatta, Ngina Kenyatta aliolewa katika harusi ya kitamaduni.

Kulingana na picha zilizosambazwa na marafiki wa karibu waliohudhuria harusi hiyo, mada ya harusi ya Ngina ilikuwa mavazi ya Kiafrika, na rangi ya bluu ilitawala hafla hiyo.

Miongoni mwa waliohudhuria harusi hiyo ni Waziri wa Afya Mutahi Kagwe.

Mamake Uhuru Kenyatta Mama Ngina pia alihudhuria hafla hiyo.

Alivaa kofia maridadi ya zambarau na mavazi ya Kiafrika yenye maua yanayolingana na mkufu wa lulu.

Alikuwa amechumbiwa na Alex Mwai, mtoto wa meneja mkuu wa Klabu ya Karen Sam Mwai.

Maelezo kuhusu harusi ya Ngina yalifichuliwa na Dennis Itumbi kupitia mtandao wake wa kijamii.

Mnamo 2021, Ngina alikuwa katika hospitali moja jijini Nairobi, ambapo alijifungua mtoto wake wa kwanza.