Mbunge wa Mathira na Mwakilishi wa wanawake wa Murang'a wafichua wanachumbiana

Wabunge hao wa muhula wa kwanza walithibitisha wanachumbiana siku ya Alhamisi

Muhtasari

•Betty alimtakia mbunge huyo wa Mathira heri ya siku ya kuzaliwa kupitia akaunti yake ya Facebook ambapo alimwita  'mpenzi'.

•Wakenya wanaoonekana kupendezwa na maendeleo hayo mapya wamekuwa wakiwapongeza wawili hao tangu walipotangaza.

Mbunge wa Mathira Eric Mwangi na Mwakilishi wa wanawake wa Murang'a Betty N Maina
Image: FACEBOOK// BETTY N MAINA

Mwakilishi wa Wanawake wa kaunti ya Murang'a Betty Maina na Mbunge wa Mathira Eric Mwangi Wamumbi ni wachumba rasmi.

Wabunge hao wawili wa muhula wa kwanza walitangaza mapenzi yao hadharani siku ya Alhamisi, Desemba 21  wakati Eric alipokuwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa. Eric alikuwa akisherehekea kutimiza miaka 35.

Betty alimtakia mbunge huyo wa Mathira heri ya siku ya kuzaliwa kupitia akaunti yake ya Facebook ambapo alimwita  'mpenzi'.

"Miaka 35 ni mafanikio makubwa. Ishi kwa muda mrefu mpenzi wangu," Betty aliandika.

Mwakilishi wa wanawake huyo wa Murang'a aliambatanisha ujumbe huo na picha nzuri yake na Eric wakitazamana huku mahaba mazito yakiwa yameandikwa kwenye nyuso zao. Pichani, wote wawili walikuwa wamevaa nguo nyeusi.

Video ya viongozi hao wawili wakicheza densi pamoja kwa furaha katika hafla iliyohudhuriwa na watu kadhaa pia imeibuka. Kuna tetesi zisizothibitishwa kuwa Eric tayari amemvisha pete ya uchumba Betty na wamechumbiana.

Wakenya wanaoonekana kupendezwa na maendeleo hayo mapya wamekuwa wakiwapongeza wawili hao tangu walipotangaza.

MC Jimmie Kajim: Hongera watu wangu Betty N Maina na Eric Mwangi Wamumbi.

Hon Reagan: Mapenzi yanashinda. Hongera Mwakilishi wa wanawake wa Muranga Betty N Maina na Mbunge wa Mathira Eric Mwangi Wamumbi.

Martha JM Miano: Mathira yakutana na Murang'a. Hongera Mbunge wa Mathira Eric Mwangi Wamumbi na Mbunge wa Kaunti ya Murang'a Betty N Maina. Mapenzi yanashinda.....❤

Muyu KE: Hongera Eric Mwangi Wamumbi na Betty N Maina, Apataye mke anapata kitu chema, na anajipatia kibali kwa Mungu. Mnaonekana wazuri pamoja.

Shiku Smart:Hongera sana 🎊 Mhesh Betty N Maina hii imeenda nimefurahi kwako mpenzi, mapenzi ni matamu.