Peter Miracle Baby aeleza kwa nini anataka kuwa pasta na kuhubiri injili baada ya kupona

“Najua Mungu akitaka, atanipa eneo la kuweka kanisa na litakua, nikishapata eneo la kuweka kanisa, najua waumini watakuja kwa kweli. Kwa hiyo, yangu nimeianza kupitia muziki,” Miracle Baby alisema.

Msanii wa Gengetone na Mugithi
Peter Miracle Baby// Msanii wa Gengetone na Mugithi
Image: Facebook

Msanii wa Mugithi na Gengetone, Peter Miracle Baby amefunguka kwamba angependa sana kubadili taaluma yake na kuwa muhubiri kueneza injili baada ya kupambana na ugonjwa kwa Zaidi ya mieizi 3 sasa.

Akizungumza na KOM, kijana huyo alioomba kabla ya mahojiano aanze na maombi, jambo ambalo alilifanya na kusema kwamba nia yake ni kuwa mhubiri.

Miracle Baby ambaye amekuwa katika safari ndefu ya matibabu kutokana na kile mkewe Carol Katrue alisema ni kupasuka kwa utumbo wake mdogo alisema kwamba ni nadhiri ambayo aliiweka kwamba pindi atakapopona, ataanza kueneza injili.

Hata hivyo, alisema kuwa kuhubiri kuko katika njia nyingi, akisema kuwa yeye kwa sasa hana kanisa na pengine huenda ataanza kuhubiri kupitia nyimbo.

“Nilisema nataka kuwa pasta na kuhubiri, unanielewa. Lakini kuhubiri kuko katika njia nyingi, mtu unaweza kuhubiri kupitia nyimbo, kwa sababu mtu kama mimi kwa sasa sina kanisa, wala sina eneo la kuweka kanisa,” Miracle Baby alisema.

Msanii huyo aidha alionesha Imani yake kuu kwamba Mungu atamfungulia njia na milango kupata eneo la kuanzisha kanisa, akionesha matumaini makubwa katika kufanikiwa katika mkondo huo mpya.

“Najua Mungu akitaka, atanipa eneo la kuweka kanisa na litakua, nikishapata eneo la kuweka kanisa, najua waumini watakuja kwa kweli. Kwa hiyo, yangu nimeianza kupitia muziki,” Miracle Baby alisema akitolea mfano wa wimbo mpya ‘Ndi Mwihia’ ambao wameutoa juzi na mkewe, Carol Katrue.

Msanii huyo akizungumzia safari ya tatizo lake la tumbo, alisema kwamba alianza kupata tatizo la kuumwa na tumbo mwaka 2018.

Mapema mwaka huu, hali hiyo ilikuwa mbaya Zaidi kupelekea kulazwa kwake, jambo lililopelekea hatua za upasuaji wa Zaidi ya mara 3 ndani ya mwezi mmoja tangia Januari.

 

Msanii wa Gengetone na Mugithi
Peter Miracle Baby// Msanii wa Gengetone na Mugithi
Image: Facebook