“Mungu ameniwezesha kula tena” – Miracle Baby asema baada ya kipindi kigumu cha ugonjwa

Baada ya kipindi cha kulazwa hospitalini, Miracle Baby alifanyiwa upasuaji mara tatu katika kipindi cha mwezi mmoja na hivi majuzi alisema kwamba ana’miss sana kujiendea chooni mwenyewe bila msaada.

Muhtasari

• Miracle Baby na mpenzi wake Carol Katrue walipelekwa katika ziara ya likizo Mombasa na kampuni moja ya usafiri wa watalii humu nchini.

• Miracle Baby amekuwa akipambana na ugonjwa tangu mapema Janauri mwaka huu katika hali ambayo mpenzi wake alisema ni matatizo katika utumbo wake.

miracle baby
miracle baby
Image: facebook

Msanii wa Mugithi na Gengetone, Peter Miracle Baby ameendelea kuwapa sasisho mashabiki wake kuhusu hali yake ya ugonjwa.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Miracle Baby alifichua kwamba afya yake inaendelea kuimarika na kwamba kwa mara ya kwanza baada ya kipindi kirefu, ameweza kula chakula tena.

Miracle Baby na mpenzi wake Carol Katrue walipelekwa katika ziara ya likizo Mombasa na kampuni moja ya usafiri wa watalii humu nchini.

Akiwa huko Mombasa, alichapisha picha akiwa anakula na kusema kwamba kwake aliona kitendo hicho kama muujiza kwani imekuwa muda sasa hajaweza kujilisha mwenyewe chakula kigumu.

Alimshukuru Mungu kwa hatua za kuimarika kwake kiafya na kusema kwamba kama ameweza kumrejeshea afya na hamu ya chakula, ataweza kumsaidia pia mtu yeyote mwenye matatizo.

Mungu abaki kuitwa Mungu kama ameniwezesha kukula tena akii pia wewe atakusaidia ... Na Zunguka Africa Safaris LTD mbarikiwe tena saana kunileta Mombasa,” alisema huku akishukuru kampuni hiyo kwa kumpeleka Pwani.

Miracle Baby amekuwa akipambana na ugonjwa tangu mapema Janauri mwaka huu katika hali ambayo mpenzi wake alisema ni matatizo katika utumbo wake.

Baada ya kipindi cha kulazwa hospitalini, Miracle Baby alifanyiwa upasuaji mara tatu katika kipindi cha mwezi mmoja na hivi majuzi alisema kwamba ana’miss sana kujiendea chooni mwenyewe bila msaada.

Wakati wa kusherehekewa siku yake ya kuzaliwa, Miracle Baby alisema kwamba anatumai hivi karibuni ataanza kujiendea choo mwenyewe, kwani ni jambo ambalo angependa kujifanyia na si kusaidiwa kama ambavyo anasaidiwa katika hali yake ya ugonjwa.

“Wakati nawaona nyinyi watu kutoka St Mary’s, moyo wangu hudunda kwa furaha. Moyo unadunda kwa sababu ninapowaona, najiona mwenyewe nikienda chooni hivi karibuni. Nimemiss kwenda chooni, na huu si mzaha,” Miracle Baby alisema.

“Mnaweza tafakari kutoka Janauri, sijakuwa na uwezo wa kuenda chooni lakini hivi karibuni nitapata kurudishiwa utumbo wangu kwa njia sawia ili nijiendee chooni,” aliongeza.