“Nime’miss kuenda chooni!” – Msanii wa Mugithi, Peter Miracle Baby

“Wakati nawaona nyinyi watu kutoka St Mary’s, moyo wangu hudunda kwa furaha. Moyo unadunda kwa sababu ninapowaona, najiona mwenyewe nikienda chooni hivi karibuni. Nimemiss kwenda chooni, na huu si mzaha.”

Muhtasari

• Msanii huyo amekuwa katika hospitali tangu katikati ya mwezi Janauri na mpenzi wake amekuwa akiongoza baadhi ya watu kutoa michango yao kwa ajili ya matibabu yake.

MIRACLE BABY
MIRACLE BABY
Image: facebook

Msanii wa Gengetone na Mugithi, Peter Miracle Baby amefichua kwamba kitu kimoja ambacho amekikosa katika maisha yake tangu kuanza kulazwa Januari mwaka huu ni kuenda msalani peke yake pasi na kusaidiwa na mtu.

Akizungumza wakati wa tafrija ya siku yake ya kuzaliwa iliyoabdaliwa na marafiki wake wa karibu, Miracle Baby alisema kwamba anapowaona watu ambao wamekuwa wakimshughulikia haswa hospitalini, anajiona akienda chooni.

Msanii huyo ambaye mpenzi wake Carol Katrue alifichua kwamba ana matatizo ya kupasuka kwa utumbo mdogo uliopelekea yeye kufanyiwa msururu wa upasuaji hadi mara 3 ndani ya mwezi mmoja, alisema kwamba anatamani kupona ili kuweza kujipeleka mwenyewe chooni.

“Wakati nawaona nyinyi watu kutoka St Mary’s, moyo wangu hudunda kwa furaha. Moyo unadunda kwa sababu ninapowaona, najiona mwenyewe nikienda chooni hivi karibuni. Nimemiss kwenda chooni, na huu si mzaha,” Miracle Baby alisema.

“Mnaweza tafakari kutoka Janauri, sijakuwa na uwezo wa kuenda chooni lakini hivi karibuni nitapata kurudishiwa utumbo wangu kwa njia sawia ili nijiendee chooni,” aliongeza.

Msanii huyo amekuwa katika hospitali tangu katikati ya mwezi Janauri na mpenzi wake amekuwa akiongoza baadhi ya watu kutoa michango yao kwa ajili ya matibabu yake.

Itakumbukwa kwamba kwa wakati mmoja mwanaharakati Eric Omondi alisimama na familia hiyo kwa kuwachangishia Zaidi ya shilingi milioni moja kwa matibabu baada ya ripoti kuibuka kwamba alikuwa amekwama hospitalini.