"Karibu kwenye ghorofa ya tatu" Diana Marua amsherehekea mumewe Bahati kimahaba

Bahati anasherehekea kutimiza miaka 30.

Muhtasari

•Bahati ambaye anasherehekea kutimiza miaka 30 duniani ameitaja siku hii kuwa siku kubwa katika maisha yake.

•Diana alimtaja kuwa mume wake, mfalme wake, mshirika wake wa maombi, nguvu zake, nguzo yake na baba wa watoto wake.

Diana Marua na mumewe Bahati
Image: INSTAGRAM// DIANA MARUA

Hivi leo, Desemba 23, mwimbaji mashuhuri Kelvin Kioko almaarufu Bahati anaadhimisha siku ya kuzaliwa kwake.

Bahati ambaye anasherehekea kutimiza miaka 30 duniani ameitaja siku hii kuwa siku kubwa katika maisha yake.

"Hatimaye, Bahati ako na miaka thelathini. Leo ninasherehekea siku yangu ya kuzaliwa ya 30. Leo ni siku yangu kuu. Nilizaliwa 22 dec 1992," aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Mke wake Diana Marua alimkaribisha katika umri wa 30's na kumsherehekea kwa hatua ambayo amepiga. Alimtaja kuwa mume wake, mfalme wake, mshirika wake wa maombi, nguvu zake, nguzo yake na baba wa watoto wake.

"Ninakusherehekea kila siku lakini leo ni siku maalum kwa sababu ni siku yako ya kuzaliwa 🎉 KARIBU KWENYE GHOROFA YA TATU MPENZI @BAHATIKENYA ❤️," Diana Marua alimwandikia mumewe kwenye Instagram.

Aliongeza, "Zawadi kubwa zaidi ni kuwa nawe kila siku na kukuona katika 30 ukiwa mchangamfu, mwenye furaha na umetosheka. Huwa inanipa furaha na amani."

Mama huyo wa watoto watatu alimtakia Bahati furaha tele maishani, mafanikio mengi, baraka na neema ya Mungu.

Pia alimhakikishia kuhusu upendo wake mkubwa kwake na kumweleza jinsi huwa anamuombea mara nyingi.

"Matamanio ya moyo wake yatimizwe kwa Jina la Yesu. HERI YA SIKU YA 30 YA KUZALIWA MFALME WANGU ... KWA DAIMA NA MILELE. NAKUTHAMINI ❤️‍🔥❤️‍🔥❤️‍🔥❤️‍🔥," Alisema rapa Diana B.

Diana Marua alitimiza miaka 33 mwezi uliopita.