Walidhani hatuwezi kulipa - Bahati na Diana wasema walikatazwa kununua nyumba

Bahati na mkewe Diana Marua walifichua kwa nini walikatazwa kununua nyumba

Muhtasari

• Marua alisema kuwa wenye nyumba walidai kuwa wanakaa wadogo na wataleta kelele.

 

Bahati na Diana Marua
Image: INSTAGRAM// BAHATI

Wanandoa Bahati na Diana Marua walidai kuwa walikatazwa kununua nyumba za kifahari walipokuwa kwenye harakati ya kutafuta nyumba.

Kwenye YouTube, Diana Marua alisema kuwa walijaribu kununua nyumba huko Kiambu Road ila hawakuruhusiwa.

Alisema kuwa wenye nyumba walidai kuwa wanakaa wadogo na wenye kuleta sherehe na kupiga kelele.

"Tukifika kwenye benki ili tuweze kulipia nyumba hiyo, tulipigiwa na wenye nyumba kisha kuambiwa kuwa tunakaa wenye kufanya sherehe kila siku, na kuulizwa iwapo tutaweza kulipia," Bahati alisema huku akiigiza sauti ya mtu mwingine.

Marua alisema walijaribu kuwaeleza kuwa yeye na mume wake wana watoto na si watu wa sherehe kila siku.

Bahati pia alisema sababu ya kukatazwa kununua nyumba hiyo  ni kuwa alitaka  kuirembesha lakini mwenye nyumba alikataa na kusema kuwa wataharibu nyumba.

Hata hivyo, hatimaye, Bahati alipata nyumba baadaye ambayo ndiyo aliyomzawadi mkewe siku ya wapendanao.

Nyumba hiyo ambayo ni ya kifahari inadaiwa kuwa ya thamani ya milioni 27.  

Kando na nyumba, mwanamuziki huyo pia alimzawadi mkewe gari na shamba kusherehekea mapenzi yao.

Diana alimshukuru sana mumewe kwa zawadi ya nyumba hiyo huku akisema kuwa ndiyo zawadi bora zaidi ya Valentines ambayo amewahi kupokea.