Diana Marua ajivunia kukutana na mpenzi wa mwanawe, Morgan Bahati

Diana alisema kuwa anajivunia Morgan na akamhakikishia kuhusu upendo wake kwake

Muhtasari

•Diana alionekana mwenye kujivunia sana mtoto wake katika picha zote ambazo alipiga na kuchapisha.

•Diana aliionekana akimsaidia Morgan kujiandaa na kukusanya ujasiri kabla ya kukutana na mpenziwe.

Mtoto wa kulea wa Bahati na mke wake Diana Marua, Morgan Bahati alihitimu siku ya Jumamosi baada ya kufanya mitihani yake ya KPSEA.

Huku akimsherehekea kwa mafanikio hayo, Diana alisema kuwa anajivunia mwanawe na akamhakikishia kuhusu upendo wake kwake.

"Ninajivunia kuitwa mama yako. Imekuwa ni safari na kukuona ukihitimu siku ya leo, nimeshangazwa na uaminifu wa Mungu. Nakupenda Morgan Bahati," alisema kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Mama huyo wa watoto watatu pia alichapisha picha na video kadhaa ambazo alichukua wakati wa kwa hafla hiyo ya kuhitimu  iliyofanyika katika Juja Preparatory School  ambapo Morgan amekuwa akisomea. Alionekana mwenye kujivunia sana mtoto wake katika picha zote ambazo alipiga na kuchapisha.

"Morgan ana haya kwamba ninamrekodi, lol," alisema chini ya video iliyomuonyesha Morgan na wenzake wakidensi.

Katika video nyingine aliyochapisha, mke huyo wa Bahati  alifichua kwamba alikutana na mpenzi wa mtoto wake. 

Videoni, alionekana akimsaidia Morgan kujiandaa na kukusanya ujasiri kabla ya kukutana na mpenziwe ambaye hajafichuliwa.

"Leo nimeona mambo hii shule.. ooh na nilikutana na mpenzi wa @morgan_bahati leo. Vlog inakuja," Diana alisema.

Katika video hiyo iliyorekodiwa jioni, Morgan alikuwa amevalia suti nzuri nyeusi ,shati jeupe na kiatu cheupe.

"Drip, drip kijana wangu. Unakaa vizuri," Diana alimwambia.

Sik chache zilizopita, Bahati alimtia moyo mwanawe huyo na kumtakia mafanikio  huku  huku akijiandaa kufanya mtihani wake kitaifa wa darasa la sita.

Mwimbaji huyo alihudhuria hafla ya kuwaombea watahiniwa na kusema  kuwa ana matumaini Morgan atafaulu kwenye mtihani huo wake wa kwanza wa kitaifa.

"Nikitazama jinsi tulivyotoka mbali, siwezi kuamini kuwa mwanangu ni mtahiniwa mtarajiwa wa mtihani wa kitaifa wa darasa la sita. Utukufu kwa Mungu unapojitayarisha kujiunga na Junior High," Bahati alisema.

"Ni Mungu tu anafahamu safari yetu. Ninajua kuwa utakuwa mtu bora kwenye maisha  na siku moja utahamasisha dunia kwa hadithi yako. Nakupenda Morgan Bahati," aliandika.