Bahati amwandikia mwanawe wa kuasili ujumbe akisubiri kufanya mtihani wa kitaifa

Morgan ni mtahiniwa wa mtihani wa kitaifa wa Grade 6

Muhtasari

• Bahati alisema jinsi anajivunia mwanawe ambaye anajitayarisha kuufanya mtihani wa kitaifa.

• "Ni Mungu tu anafahamu safari yetu. Ninajua kuwa utakuwa mtu bora kwenye maisha  na siku moja utahamasisha dunia kwa hadithi yako. Nakupenda Morgan Bahati," Bahati aliandika.

Morgan na Bahati
Image: Bahati Instagram

Mwanamuziki Bahati amemwandikia mwanawe wa kuasili Morgan Bahati ujumbe huku akijitayarisha kufanya mtihani wake kitaifa wa darasa la sita.

Staa huyo wa muziki alikuwa amehudhuria hafla ya kuwaombea watahiniwa ili kumtakia mema.

Kwenye Instagram, Bahati alisema kuwa ana matumaini Morgan atafaulu kwenye mtihani huo wa gredi ya sita.

"Nikitazama jinsi tulivyotoka mbali, siwezi kuamini kuwa mwanangu ni mtahiniwa mtarajiwa wa mtihani wa kitaifa wa darasa la 6. Utukufu kwa Mungu unapojitayarisha kujiunga na Junior High," Bahati alisema.

"Ni Mungu tu anafahamu safari yetu. Ninajua kuwa utakuwa mtu bora kwenye maisha  na siku moja utahamasisha dunia kwa hadithi yako. Nakupenda Morgan Bahati," aliandika.

Mashabiki wake walimpongeza kwa kuwa mzazi bora kwa Morgan huku wengine wakimtakia Morgan mfanikio kwenye mtihani wake.

"Wewe ni bora kati ya watu milioni, watu wanakuhukumu ila hawawezi kuwachukua na kuwapanga watoto wa mitaani ama hata kuwalisha. Wanachofanya ni kushika simu zao na kuandika upuzi," nyachworosedesire alisema.

"Huyu Bahati Mungu ampe maisha marefu. Watu wengine wana tatizo la kuwachukua na kuwaruhusu watu wafamilia yetu kuishi kwao hata kwa siku moja. Ni shida sana ila yeye anapanga na hata si mmoja,"nyawira1324 aliandika.

"Unaona sasa kidogo mtoshane urefu, hata hivyo nakutakia mema Morgan Bahati,"kiemewambogo alisema.

"Kazi safi, hongera sana kwa kijana mdogo Morgan."Mwanaume anayetaka kuongoza lazima ajivunie matokeo yake" Hiyo ni kwako, jijazie," wachiramachariaofficial aliandika.

Watahiniwa wanatarajiwa kuanza mtihani wao wa kitaifa wiki   ijayo  tarehe 28 Novemba.