Diana Marua ampongeza Bahati kwa kuwa baba anayejitahidi

Marua alisema kuwa Bahti amemsaidia kwenye malezin ya watoto wao

Muhtasari

• Marua alisema kuwa Bahati amejishindia mapendeleo ya watoto wao kwani chochote wanachohitaji au kuitisha wanapewa.

Bahati na mtoto wake

Diana Marua amemshukuru mume wake Bahati kwa kuwa baba anayejitahidi kuwalea wanao.

Kwenye Instagram, Diana alimwandikia mume wake ujumbe huku akieleza jinsi alivyojitahidi kuwa baba mzuri.

"Siwezi kutaka kuwa na kitu kingine chochote ila wewe kuwa baba ya watoto wangu. Kama kuna mtu ambaye watoto wetu wanafurahia kuwa karibu nao ni wewe," Marua alisema.

Alisema kuwa Bahati amepata upendo wa watoto kwani chochote wanachohitaji au kuitisha wanapewa.

Jambo hilo limefanya Marua kuwa mzazi anayejulikana kuwa mkali na watoto wake.

"Asante kwa kunifanya kuonekana kuwa mzazi 'mbaya' wakati mwingine. Hakuna peremende kwa nyumba na nimenena! Tunakupenda baba yetu Bahati Kenya," aliandika.

Wawili hao walimpokea mtoto wao wa kike hivi majuzi na mwanamuziki huyo amekuwa akijikakamua kumsaidia Marua kumlea.

Bahati amekuwa akipakia picha akimlea mtoto wake mchanga.

"Wakati mwingine nikihitaji miujiza, ninamwangalia binti yangu machoni kisha nafahamu kuwa nina miujiza tayari!" Bahati aliandika huku kwenye picha akimbusu binti yake.

Hivi majuzi, wanandoa hao walitangaza kuzaliwa kwa binti yao Jumanne tarehe 1 mwezi wa Novemba na kumpa jina Malakia Nyambura Bahati.

Wawili hao walipokea jumbe za heri njema mitandaoni kutoka kwa mashabiki wao wakiwemo watu mashuhuri.

Marua alikuwa amesubiriwa kwa hamu na mashabiki wake kujifungua huku wengine wakishuku kuwa alijifungua kitambo na alikuwa akitafuta kiki.

Bahati pia amekuwa akitumia wakati wake kuwalea watoto wake wengine Majesty na Heaven akiwafunza mambo kama kucheza piano.