Sikuwa na shida ya pesa!Diana Marua asimulia maisha yake ya nyuma

Diana alifichua kuwa na wapenzi tofauti waliomlipia nyumba, kumnunulia vitu vya thamani kama nguo na kumpeleka out.

Muhtasari

• Mama huyo wa watoto watatu alisema vile alikuwa na wapenzi wengi waliokuwa wanamtimizia mahitaji yake yote ya kibinafsi. 

• Alifichua kuwa kwenye uhusiano na mwanamume aliyekuwa kwenye ndoa na alikuwa akimpenda kwa dhati.

Diana Marua

Rapa Diana Marua amegeuka gumzo mtandaoni baada ya video yake akieleza jinsi alivyoweza kujikimu kabla ya kuoana mwanamuziki Bahati.

Mama huyo wa watoto watatu alisema vile alikuwa na wapenzi wengi waliokuwa wanamtimizia mahitaji yake yote ya kibinafsi. 

Alisema kwamba alikuwa akibadilisha magari kila siku na maisha yake yalikuwa shwari kwani hakuwa anafanya kazi yoyote lakini pesa alikuwa akipata.

"Nilikosa mahitaji maishani mwangu nikaanza kuwa kwenye mahusiano na wanaume wengi kwa wakati mmoja.Nilitaka maisha mazuri, kitu ambacho nilitaka zaidi ilikuwa pesa. Pesa kwangu haikuwa shida," Diana alisema.

Diana alifichua kuwa na wapenzi waliomlipia nyumba, kumnunulia vitu vya nyumba, nguo na hata kumpeleka out.

Alisema kuwa siku za kwanza za kujuana na Bahati, mwanamuziki huyo alimuuliza maswali kuhusu alivyokuwa anabadilisha magari kila wakati.

Alisema Bahati alijuwa hakuwa anafanya kazi ila hakukosa chochote, na kuvalia mavazi ya bei ghali.

"Nilikuwa nikikutana na Bahati, leo nina gari hili, kesho ni lingine. Nilikuwa na kila kitu... Kuna mtu alikuwa ananipa elfu 10, mwingine elfu 30 huku mwingine ananipa elfu 20," alisimulia.

Alisema pesa hizo alitumia kujinunulia vitu; mavazi, chakula, viatu, alikuwa na kila kitu alichohitaji.

Alifichua kuwa kwenye uhusiano na mwanamume aliyekuwa kwenye ndoa na alikuwa akimpenda kwa dhati. Mwanamume huyo aliahidi kumnunulia gari na nyumba na  kumzalisha mtoto mmoja.

"Siwaambii haya kwa kutaka kujigamba, nawaambia ili kuwagusa na kuwapa moyo ili mbadilike. Nilikuwa najiuliza iwapo hayo maisha yalikuwa bora kwangu. Nilijiuliza kwamba nikiolewa mbeleni nitakuwa mwenye amani kuhusu maisha yangu ya zamani," Marua alisema.