Anerlisa Muigai azungumzia maisha ya zamani ya Diana Marua

Anerlisa alisema watu wataanza kujadili idadi ya wanaume alioshiriki nao mapenzi.

Muhtasari

• Muigai alisema kuwa Diana hangefunguka kwa wakati huu ambao amekuwa mtu maarufu na hata kupata mume ambaye anampenda kwa dhati.

• "Mambo yako ya zamani wakati mwingine yanaweza kuwafanya watu kuwa na mtazamo tofauti kukuhusu  hata kama ulifanya hivyo kuwasaidia watu," Muigali alisema.

Anerlisa muigai, Diana Marua

Mjasirimali Anerlisa Muigai ametoa maoni yake kuhusu maisha ya zamani ya Diana Marua baada ya kufichua mengi kuhusu mienendo yake.

Muigai anasema maisha ya zamani ya mtu yanafaa kusalia ya kibinafsi na hayafai kuyazungumziwa.

Hata hivyo alisema hana sababu ya kumkosoa Diana ambaye sasa ni mkewe mwanamuziki Bahati.

"Sina chochote dhidi ya Diana, mimi ni mmoja wa watu wanaomshabikia kama mama lakini kwa nini akaamua kuzungumza sasa hivi? Ukweli wa kusikitisha ni kwamba watu wataenda moja kwa moja kuzungumzia idadi ya wanaume alioshiriki nao mapenzi," alisema.

Alisema kuwa Diana hangefunguka kwa wakati huu ambao amekuwa mtu maarufu na hata kupata mume ambaye anampenda kwa dhati.

Muigai aliongeza kuwa sababu nyingine ambayo Marua hangefunguka ni kuwa yeye sasa ni mama wa watoto watatu ambao wanahitaji kulelewa na maadili mema.

"Mambo yako ya zamani wakati mwingine yanaweza kuwafanya watu kuwa na mtazamo tofauti kukuhusu  hata kama ulifanya hivyo kuwasaidia watu," Muigali alisema.

Alisema kama ni lazima kuwahadithia watu kuhusu maisha ya zamani basi ushauri wake ni kuwa angetumia rafiki kueleza jambo hilo.

Hii ni baada ya video ya Marua ya miaka miwili iliyopita akieleza maisha yake ya zamani kusambaa.

Alifichua kuwa kwenye uhusiano na mwanamume aliyekuwa kwenye ndoa na alikuwa akimpenda sana. Mwanamume huyo aliahidi kumnunulia gari na nyumba na kumzalisha mtoto mmoja.

"Nilikuwa nikikutana na Bahati, leo nina gari hili, kesho ni lingine. Nilikuwa na kila kitu... Kuna mtu alikuwa ananipa elfu 10, mwingine elfu 30 huku mwingine ananipa elfu 20," alisimulia.