Bahati ataka kujua mbona hajafanana na mkewe licha ya kupendana kwa muda mrefu

Alisema kuwa huenda dhana ya wawili kufanana baada ya kupendana kwa muda ni uongo.

Muhtasari

• Niliambiwa Tukipendana Tutaanza Kufanana.... Wasee Mbona Sijakua Mweupe Kama Diana Marua? - Bahati aliuliza.

Bahati na mkewe Diana Marua.
Bahati na mkewe Diana Marua.
Image: Instagram

Bahati Kioko, msanii wa Kenya amepinga kauli kuwa watu wawili wapendanao wakiishi pamoja kwa muda mrefu hatimaye huanza kufanana.

Msanii huyo alipakia picha kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa na mkewe ambapo alisema kuwa huenda dhana hiyo ni uongo huku akitoa maelezo ya kutetea na kuongeza uzito kwenye kauli yake.

Kulingana na Bahati, yeye amekaa na Diana Marua kwa miaka mingi lakini bado hajaona kama sura yake inakuwa nyeupe na kufanana na mkewe Marua ambaye weupe wake ni wa mchuzi wa kunde.

Niliambiwa Tukipendana Tutaanza Kufanana.... Wasee Mbona Sijakua Mweupe Kama @Diana_Marua ??? 🤩” Bahati aliuliza kwa utani.

Mkewe Diana Marua alimtoa wasiwasi kwa kumhimiza kuwa huenda kwa sura ya nje hajafanikiwa kuwa mweupe lakini upendo wake kwake kutoka ndani mwake ni mweupe kama theluji.

“Nafsi yako ya ndani ni nyepesi na nyeupe kuliko mimi. Tosheka na hiyo mpenzi wangu #ABEBO ️” Marua alimwambia huku akiweka emoji za kucheka.

Wapenzi hao wanazidi kuweka viwango vya mapenzi ya mitandaoni kuwa ghali zaidi haswa kwa jinsi wanavyodekezana na kupetiana peti kwenye mitandao ya kijamii bila haya wala woga.

Pamoja, wamebarikiwa kuwa na watoto watatu, wa hivi punde akiwa nib inti kwa jina Malaika.

Licha ya kuwa na mapungufu yao ambayo yanajulikana hadharani, maneno ya watu hayajafanikiwa kuyumbisha uhusiano wao, hsawa ile kashfa ya hivi karibuni iliyoibuliwa na watumizi wa Twitter waliorejelea video ya kitambo Diana akisimulia pande nyeusi ya maisha yake.

Wengi walimtaka Bahati kuandika talaka tatu na kumkabidhi Diana lakini alisimama tisti kama ukuta wa Berlin upande wa faraja ya mkewe na kuwa nguzo imara kwa kusema kuwa hawezi kushauriwa wala kuambiwa chochote cha kufanya na ndoa yake kwani wanaong’aka hivyo hawajui kilichomvutia kwa Marua, pengine ni hiyo hulka yake ya kuwa na wanaume wengi.