Hongera! Mwanasoshalaiti Vera Sidika ajifungua mtoto wa pili kwa siri

Vera tayari amejifungua na video alizoonyesha Alhamisi hazikuwa za moja kwa moja.

Muhtasari

•Vera alijifungua siku chache zilizopita lakini bado hajatangaza kuzaliwa kwa mtoto wake wa kiume kwa sababu ya filamu ya maisha halisi anayoigiza kwa sasa.

•“Vera angeweza kuwa hapa, lakini amejifungua mtoto tu. Sonal Merali yupo India kwa masuala ya familia,” Lisa alijibu kwa unyoofu.

Image: INSTAGRAM// VERA SIDIKA

Mwanasoshalaiti maarufu Vera Sidika alishangaza taifa siku ya Alhamisi kwa karamu ya kifahari ya kufichua jinsia ya mtoto wake wa pili.

Walakini, sasa tunapokea habari kuwa Vera tayari amejifungua na video alizoonyesha Alhamisi hazikuwa za moja kwa moja.

Vera ni mahiri sana linapokuja suala la kiki na biashara ya sanaa, iko kwenye damu yake na amethibitisha hili mara kwa mara.

Vera alijifungua siku chache zilizopita lakini bado hajatangaza kuzakliwa kwa mtoto wake wa kiume na Brown Mauzo kwa sababu ya filamu ya maisha halisi anayoigiza kwa sasa.

Kama huamini, wakati wa karamu ya maonyesho ya Real Housewives Of Nairobi kwa kipindi cha tatu iliyofanyika katika Lifestyle Gigiri (huandaliwa kila Alhamisi), mshiriki Lisa Christoffersen alimwaga mtama kwa bahati mbaya au kimakusudi.

Alipoulizwa kwa nini washiriki wengine wa kipindi cha maisha halisi hawakujitokeza kwenye karamu hiyo, Lisa alijibu kwa kufichua kwamba Sonal alikuwa nje ya nchi huku mwanasoshalaiti huyo akiwa amepokea baraka ya mtoto.

“Vera angeweza kuwa hapa, lakini amejifungua mtoto tu. Sonal Merali yupo India kwa masuala ya familia,” Lisa alijibu kwa unyoofu.

Kwa hivyo, Vera akichapisha video za kufichua jinsia ya mtoto sasa baada ya kurekodiwa awali kwa ajili ya shoo hiyo inaonyesha wazi kuwa yeye ni bingwa katika kupotosha na atafanya watu kuzungumzia anachotaka wakati anapotaka.

Chanzo cha karibu karibu na wanandoa hao mashuhuri pia kilifichua kuwa hakika Vera si mjamzito tena na alijifungua mtoto wa kiume kwa mafanikio.

Chanzo hicho kilibainisha kuwa mwanasosholaiti huyo alikuwa akifuata maandishi ya shoo na hajaweza kutangaza kuzaliwa kwa mwanawe bado.

"Vera na Mauzo walimkaribisha mtoto wao wa pili hivi majuzi, kama siku moja au mbili zilizopita, na wamekuwa wakifanya siri."

Aliongeza, "Lakini kwa kuwa anafuata maandishi ya kipindi cha uhalisia, lazima anyamaze kimya hadi itakapoonyeshwa kwa TV."

 Kwa mtindo wa kweli wa Vera, alijifungua mwanawe katika hospitali kuu ya Nairobi katika sehemu ya watu maalum kama vile ilivyokuwa na bintiye mzaliwa wa kwanza, Asia Brown.

Utafsiri: Samuel Maina