Betty Kyalo: Tulitengeneza mamilioni kutoka kwa Kyallo Kulture

Betty alidai kuwa shoo ya Real Househelps of Nairobi sio nzuri

Muhtasari

• Mfanyibiashara huyo alifichua kuwa amekuwa akichumbiana kwa karibu mwaka mmoja na amekuwa akiweka uhusiano wake kuwa wa faragha.

Image: INSTAGRAM// BETTY KYALLO

Betty Kyallo alisherehekea siku ya kuzaliwa kwake jana.

Wakati wa mahojiano na mwanasiasa maarufu Phelix Odiwuor almaarufu Jalango, Betty alizungumza kuhusu mapenzi na uhusiano, biashara, uhalisia, na jinsi walivyofichua kuwa kwa sasa wanafanyia kazi Kyallo Kulture msimu wa 2.

Kuanzia na mapenzi, mfanyibiashara huyo alifichua kuwa amekuwa akichumbiana kwa karibu mwaka mmoja na amekuwa akiweka uhusiano wake kuwa wa faragha kwani wakati huu anataka kufanya mambo tofauti na kuona jinsi mambo yatakavyokuwa.

"Ninahisi kama wakati huu nataka kufanya vitu tofauti, nataka tu kudate kwenye hali ya chini hadi niamue kuuonyesha ulimwengu kwa kuoa," alisema na kubainisha kuwa safari hii ikiwa anatembea kwenye njia sahihi, inaenda kuwa tofauti.

"Sidhani kama nitafanya harusi kubwa wakati huu kwani ni watu wawili tu." Akiongeza kuwa mapenzi ni kweli sio ulaghai kutokana na jinsi watu wengine wanavyoyachukulia na anataka tu mwanaume wake ampende bila ukaribu wa kamera.

Akimzungumzia Kyallo Kulture, mama wa mtoto mmoja alisema kuwa onyesho lao liliisha na alipata uzoefu wa kukata na shoka akifichua kuwa msimu wa kwanza ulipokelewa vyema na maoni mazuri akisema jinsi alivyoridhika na ukuaji wa dada zake kutoka kwa onyesho hilo.

"Ninahisi kama ilikuwa jukwaa nzuri kwangu na dada zangu kwani iliwapa nafasi ya kujulikana na watu wanaweza kujua nguvu zao ni nini."

Kuhusu kiasi cha pesa walichotengeneza,"tulitengeneza mamilioni kadhaa," Alisema.

Hatimaye walizungumza kuhusu biashara, alipoulizwa ni kwanini amekuwa akihamisha biashara yake kutoka eneo moja hadi jingine, mfanyibiashara huyo mwenye umri wa miaka 34 alisema kuwa anapenda miradi mipya na anapenda kuwapa wateja wake fursa na uzoefu wa ajabu na kuongeza kuwa mabadiliko ni mara kwa mara.

Alibainisha kuwa, "Nikipata eneo si zuri kwa wateja wangu, sina tatizo la kuhama na kuongeza kuwa mabadiliko ni ya mara kwa mara ikiwa unaona kitu hakifanyi kazi, unahitaji tu kuhama na kuanza upya." Pia alisema kuwa eneo jipya ni la uboreshaji na anafurahi sana kuanza safari yake mpya.

Kuhusu The Real Housewives of Nairobi, alisema kuwa kipindi hicho kina hasi na hangependa kuigizwa. "Nisingependa kuwa huko kwa vile ina sumu sana na niliitazama hata kabla haijapeperushwa." Pia alifichua kuwa anarejea kwenye Youtube kwa kuwa sasa ana maudhui ya kushangaza.