Shakilla atangaza mahari yake

Shakilla alidai kuwa lazima uwe na uwezo wa kumpeleka kwenye hoteli ya 5 star.

Muhtasari

•Shakilla alisema kuwa hawezi kuchumbiana na wanaume wa Tanzania kwa sababu wao si wa kiwango chake na pia hawana uwezo wa kuongea kiingereza vizuri.

Shakilla ashangaa wanaume kumkwepa
Shakilla ashangaa wanaume kumkwepa
Image: Instagram

Mwanasosholaiti Shakilla ameweka wazi bei ya mahari yake  kwa yule aliye na nia ya kumwoa.

Kwenye mtandao  wa Instagram, Shakilla alisema  kuwa mahari yake itakuwa shilingi milioni 15 pamoja na ngamia wapatao 100. Aliongeza kuwa lazima pia uwe na vocha ya shilingi  520,000.

Pamoja na hayo, Shakilla alisema atapewa nyumba kwa jina lake na gari la Range Rover. Pia anasema mwenye atamuoa atamlipa marupurupu ya  shilingi 195,000 kila mwezi.

Katika wakati wa maswali, shabiki mmoja alimuuliza kama anaweza kumpeleka kwenye 'lunch date'. Shakilla alijibu..."iwapo unataka kunipeleka kwenye 'date' lazima unipe shilingi elfu 13,000 na dereva wa kibinafsi".

Shakilla alisema atakayempleka amlipie vyakula na vipodozi vyake na awe na simu isiyo chini ya iPhone Promax, lazima awe mpiga picha bora na awe na uwezo wa kumpeleka kwenye hoteli ya 5 star.

Shakilla  mwenye miaka 20, amekuwa gumzo mitaani haswa baada ya kudai kwamba hakika hayuko sawa kutokana na kuburuzwa vikali mitandaoni.

Baada ya kubainisha kwamba alikuwa na uchu wa kuigiza filamu za watu wazima, baadae mwanasosholaiti huyo aliibuka tena miezi michache iliyopita akionesha wasiwasi wake kuwa hakuna mwanamume aliyetaka kuchumbiana na yeye, akihisi kwamba pengine alizaliwa kuwa mtu wa mitaani tu na wala si mke wa ndoa.

“Kwa hiyo tuseme katika wanaume wote ambao wananifuata Instagram hakuna hata mmoja anayetaka kuingia katika uhusiano wa hakika na mimi. Kwani mimi nilikusudiwa kuwa wa mitaani katika maisha yangu yote bila familia?” Mwanasosholaiti huyo aliuliza kwa wasiwasi mkubwa.

Umaarufu wa mwanasosholaiti huyo ulikua kwa kasi mwaka 2020 wakati wa janga la Covid-19 alipotambulishwa na Xtian Dela kwenye kipindi kilichonuia kuwawezesha wasanii kutumia muda wao vizuri wakati huo ambao shughuli nyingi zilisimama.