Video: Bibi harusi afyatua risasi hewani mara 4 kabla ya kutoweka

Katika video hiyo, bi harusi baada ya kumaliza kubadilishana viapo na bwana harusi, alichukua bunduki na kufyatua risasi hewani kabla ya kupotea.

Muhtasari

• Jamaa wa bibi harusi alirekodi video ya tukio hilo lililotokea usiku wa kuamkia Jumamosi kwenye nyumba ya wageni.

• Polisi walisema ni kinyume cha sheria kwa mtu kufyatua risasi hewani kama njia ya kusherehekea huku akihatarisha maisha ya watu.

Bibi harusi afyatua risasi hewani baada ya kubadilishana viapo na bwaka harusi.
Bibi harusi afyatua risasi hewani baada ya kubadilishana viapo na bwaka harusi.
Image: Twitter

Bibi harusi mmoja nchini India anatafutwa na vyombo vya dola baada ya kuchukua bunduki na kufyatua risasi hewani kabla ya kutoroka kusikojulikana.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka majarida ya nchini humo pamoja na video hiyo ambayo imeenezwa kwenye mitandao ya kijamii, bibi harusi huyo katika tukio lake kubwa alikuwa ameketi kando ya bwana Harusi.

Ghafla alipokezwa bunduki na kufyatua risasi hewani mara nne kwa mfululizo, na watu walipocharuko kila mmoja akikimbia kuokoa maisha yake kutokana na milio ya risasi, bibi harusi naye alitumia fursa hiyo kuchimba mitini asijulikane alikokwenda.

“Polisi wameandikisha kesi dhidi ya bibi harusi mwenye umri wa miaka 23 kwa madai ya kushiriki katika sherehe za kufyatua risasi siku ya harusi yake. Jamaa wa bibi harusi alirekodi video ya tukio hilo lililotokea usiku wa kuamkia Jumamosi kwenye nyumba ya wageni wilayani Hathras na kuiweka kwenye mitandao ya kijamii,” jarida moja liiripoti.

Video inayosadikiwa inamuonyesha mwanamume asiyejulikana akimkabidhi bastola bi harusi aliyefahamika kwa jina la Ragini ambaye anaonekana akifyatua risasi hewani baada ya sherehe ya kubadilishana viapo.

Msimamizi wa ziada wa Polisi Ashok Kumar alisema, "Suala hilo linachunguzwa kwa kina. Kesi ilisajiliwa dhidi ya bibi harusi kwa kukiuka kanuni zinazohusiana na sherehe za kufyatua risasi baada ya kufyatua risasi hewani mara nne wakati wa harusi yake siku ya Ijumaa."

"Yeyote anayetumia silaha kwa upele au kwa uzembe au kushiriki katika ufyatuaji risasi wa sherehe ili kuhatarisha maisha ya binadamu au usalama wa watu wengine, ataadhibiwa kifungo cha miaka miwili jela, au faini ambayo inaweza kufikia laki moja. , au zote mbili," inasomeka sehemu ya sheria za taifa hilo lenye idadi kubwa ya watu duniani.