Mavazi ya Stevo simple Boy yawaacha wengi kwa mshangao

Baadhi wamemkosoa mwimbaji huyo huku wengine wakimpongeza.

Muhtasari

•Hii ni baada ya nwanamziki huyo kutokea na mtindo wa mavazi ambao uliwashangaza wengi mtandaoni.

•Stevo Simple boy alikuwa akitangaza kibao chake mpya kwenye mtandao wake wa instagram.

STEVO SIMPLE BOY.
STEVO SIMPLE BOY.
Image: Instagram

Mwanamuziki wa Kenya Stephen Otieno Adera almaarufu Stevo Simple amewashangaza wengi mtandaoni baada ya kutokea na vazi la kushangaza akitangaza mpango wake mpya mtandaoni.

Hii ni baada ya mwanamuziki huyo kukawia bila kuachilia ngoma kutokana na tofauti zilizotekea baina yake na wasimamizi wake wa hapo awali.

Katika video aliyochapishwa kwenye ukurasa wake wa Instagram, mwimbaji huyo alionekana akiwa amevalia suruali ya jeans iliyochakaa, na kuwafanya watumiaji wa mtandao kutoa hisia mseto.

Baadhi hawakuchelewa kumkosoa rapa huyo kwa madai kuwa mavazi hayo yalimfanya aonekane mtu asiye na makazi huku wengine wakionekana kuridhishwa na mwonekano wake mpya.

Hapa ni baadhi ya maoni ya watu tofauti:

Your dresser making you look homeless man😢," Drjackolis commented.

"Stivo nakutafuta nikue designer wako unaonaje,” Peter.theelyon posted.

"Hii nayo manager amekudanganya🤣🤣🤣 unakaa Kama porcupine," Bossre2”omwami shared.

"Have now started falling for you😍😍❤🙌,” Lily75436 posted.

Now UNAKAA celeb! 🔥...” Juleschege shared.

Luku imeweza huku kwa Simpo🔥😂," Berly.b.95 posted.

"The dressing code is killing ndio manake kwa upole wake,” Fanyizin commented.