Mfululizo wa Real Housewives of Nairobi umetamatika baaada ya vipindi 12

Siku ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Susan Kaittany yaadhimisha mwisho wa RHONairobi msimu wa kwanza.

Muhtasari

• Baada ya wiki kumi na mbili za The Real Housewives of Nairobi fimau hio maaraufu kipindi cha 12 kimetamatisha msimu wa kwanza wa filamu hio.

• Fainali hiyo ilionyeshwa Alhamisi, na kisha vipindi vyote 12 vitapatikana kwenye  Showmax.

Waigizaji wa show ya Real Housewives of Nairobi.
Waigizaji wa show ya Real Housewives of Nairobi.
Image: HISANI

Baada ya wiki kumi na mbili za The Real Housewives of Nairobi fimau hio maaraufu kipindi cha 12 kimetamatisha msimu wa kwanza wa filamu hio.

Fainali hiyo ilionyeshwa Alhamisi, na kisha vipindi vyote 12 vitapatikana kwenye  Showmax.

Kipindi hiki cha mwisho kinaashiria mwisho wa sherehe ya kuadhimisha miaka 40 ya Susan Kaittany huko Malindi, na wanawake hao wazidi kukuza uhusiano wa kina baina yao.

Shoo hiyo ya The real Housewives of Nairobi ilianza kwa kishindo baada ya kuvunja rekodi za utazamaji kwa siku ya kwanza kwa filamu yoyote kwenye Showmax nchini Kenya ilipoonyeshwa kwa mara ya kwanza Februari 2023, na imeendelea kuongoza chati za Showmax na mitandao ya Twitter kwa kila toleo la vipindi vya wiki.

Wanawake wote kwenye shoo hio wametuonyesha tabia zao tofauti, waliafikia kile walichoahidi mwanzoni mwa msimu, kutoka kwa Minne Kariuki aliyetimiza matarajio ya jina lake utani la “Queen of the Shadee” hadi kwake Susan Kaittany akikumbatia urembo wake sio tu kwa mitindo yake ya nywele na fasheni lakini pia kwa namna anavyoingia, kutoka kwa Sonal Maherali akituonyesha kuwa kuongea kwa upole sio udhaifu kwa Vera Sidika kudhihirisha kuwa hata ujauzito hauwezi kua kizingiti kwake hadi kwa Lisa Christoffersen akionyesha mapenzi kwa Dr. Catherine Masitsa ukiwa wote ni kuhusu familia, pesa na biashara, na machache kuhusu drama.

unaweza kutazama vipindi vyote 12 vya The Real Housewives of Nairobi kwenye Showmax.