Njugush amposa Celestine baada ya shoo ya kusisimua nchini Uingereza

Wanandoa hawa wawili wana watoto wawili pamoja.

Muhtasari

• Celestine alieleza kwa nini baadhi ya watu walifikiri ni mzaha, lakini ilikuwa ni kweli “Tuliambiwa kwamba mapendekezo mengi yanatokea huko, kwa hiyo.”

• Baada ya tamasha yao wamerejea na kuzungumzia kuhusu upendo waliopokea kutoka kwa Wakenya nchini Uingereza.Wakiwa Uingereza,

Mchekeshaji Timothy almaarufu Njugush
Mchekeshaji Timothy almaarufu Njugush
Image: INSTAGRAM

Kampuni ya Njugush Creatives imeeneza mabawa yake hadi Uingereza, ambapo Njugush na mkewe waliwatumbuiza Wakenya wanaoishi nchini humo. 

Baada ya tamasha lao wamerejea na kuzungumzia kuhusu upendo waliopokea kutoka kwa Wakenya nchini Uingereza. Wakiwa Uingereza, Timothy almaarufu Njugush alimchumbia Celestine.

Posa hiyo ambayo imezua mjadala mitandaoni liliwasisimua mashabiki wao. Wakizungumza na vyombo vya habari katika uwanja wa ndege Jumanne, Mei 9, Njugush na mkewe walieleza sababu ya posa licha ya kuwa tayari wamefunga ndoa.

Njugush alisema “Hili limekua tatizo kwa muda sasa kuwa bado sijamposa Cellestine licha ya kufanya harusi. Inakuwa wewe unataka watoto wangapi haya juu ya tukioana ilikua kali sana, sasa kwa sababu nina uwezo wa kumchumbia cellestine. Kila mahali naenda tunapropose,"

Celestine alieleza kwa nini baadhi ya watu walifikiri ni mzaha, lakini ilikuwa ni kweli “Tuliambiwa kwamba posa nyingi hutokea huko, kwa hivyo....”

Cellestine hakupata nafasi ya kumalizia maelezo yake huku Njugush akikatiza.

"Noooo, unaharibu, unaharibu" Aliambia Cele huku akiongeza kwenye vyombo vya habari."Asante sana kwa maswali yako" Celestine pia aliongeza, "Alifanya uamuzi sahihi, labda sikupaswa kusema".