Hata mimi naweza beba hivi, ni vile tu naogopa kuwashwa na nyasi - Njugush

Nicah the Queen alipakia picha pamoja na mabinti wao wakiwa wamelala mgongoni mwa DJ Slahver.

Muhtasari

• Wanamitandao walimtaka Njugush kufanya hivyo kwa mkewe Celestine na wanao wakisema kuwa kisingizio cha kuwashwa na nyasi ni uongo.

Njugush atania picha ya Nicah mgongoni mwa DJ Slahver
Njugush atania picha ya Nicah mgongoni mwa DJ Slahver
Image: Instagram

Mwigizaji na mcheshi  Blessed Njugush amezua utani katika picha ya pamoja ya mwanamuziki wa injili Nicah the Queen akiwa amemlalia mchumba wake DJ Slahver kwenye mgongo.

Nicah alipakia picha hiyo ambayo DJ Slahver amelala chini kwa nyasi kifudifudi huku Nicah akiwa juu yake na mabinti wao wawili wakiongezea juu ya mgongo wake pia kwa njia sambamba.

Nicah alimtania mchumba wake akitaka kujua kama ana nguvu za kuwahimili wote watatu, kwa maana ya yeye na watoto wawili na hapo ndio Njugush aliamua kupeleka ucheshi wake akisema kuwa hata yeye kuwabeba watu mgongoni hivyo.

“Furaha yote katika Jina la Yesu Mwenye Nguvu! @slahverdon Uko na nguvu kweli?” Nicah aliuliza.

Njugush alisema kuwa kubeba watu hivyo si kazi ngumu lakini akasema ni vile hawezi kuhimili kwa nyasi kwa sababu atapata kujikuna kutokana na kuwashwa na nyasi zile.

Hata mimi naweza bebana hivo ni vile nitajikuna juu ya nyasi,” Njugushi alisema.

Wengi walioona komenti hiyo ya Njugush walimtag mkewe Celestine wakimtaka kumshrutisha Njugush kumbeba hivyo kwa kusema kuwa kisingizio cha kuwashwa na nyasi akijaribu kufanya vile ni uongo wa kujaribu kukwepa jukumu.

Nicah na mchumba wake DJ Slahver mwishoni mwa mwaka jana walivishana pete za uchumba katika hafla ambayo alisema mabinti zake wawili ndio waliwasaidia katika maandalizi.

Nicah aliwashtumu wengi ambao walizua maneno kuwa ndoa yake na Slahver haitaenda mbali na kuwakemea kuwa walikuwa wanamtakia mabaya kwa sababu tu yeye ni mwanamke.

Alisema kuwa tangu waachane na mchekeshaji Dr Ofweneke, mcheshi huyo amesonga mbele na maisha yake na mwanamke mwingine wala hakuwahi wasikia watu wakimsema vibaya lakini yeye kuvishwa pete ya uchumba na Slahver inawafanya wenye roho mbaya kuanza kutabiri mabaya kuhusu mapenzi yao kwa vile tu ni mwanamke anayejaribu kujitafutia ndoa.

Alisema atawashangaza sana miaka kadhaa ikipita na ndoa yake na Slahver ikuwe bado imara, hajui hao wataficha sura zao wapi.