Aliyekuwa mke wa Dr Ofweneke avishwa pete ya uchumba na mpenzi mpya

Nicah the Queen alipakia picha akivishwa pete ya uchumba na mpenzi wake wa muda mrefu, DJ Slahver.

Muhtasari

• “NILISEMA NDIYO! @slahverdon wewe na watoto wachanga mmenipata kwenye hii! Sina la kusema! Asante Bwana Yesu!” Nicah the Queen alisema.

Wachumba Nicah the Queen na DJ Slahver
Wachumba Nicah the Queen na DJ Slahver
Image: Instagram

Aliyekuwa mchumba wa mchekeshaji Dr Ofweneke, mwimbaji wa injili Nicah The Queen hatimaye amevishwa pete ya uchumba na mpenzi wake mpya mcheza santuri Slahver.

Nicah alipakia matukio hayo kwenye ukurasa wake wa Instagram na kumsifia mpenzi huyo wake kwa kuwa na ujasiri wa kumkubali baada ya kutengana na Ofweneke miaka kadhaa iliyopita.

Mama huyo wa watoto wawili alisema watoto wake wlishirikiana na Slahver kumpa bonge la ‘surprise’ hiyo kwani ni tafrija ya kipekee iliyoandaliwa pasi na yeye kujua.

“NILISEMA NDIYO! @slahverdon wewe na watoto wachanga mmenipata kwenye hii! Sina la kusema! Asante Bwana Yesu!” Nicah the Queen alisema.

Nicah the Queen na mcheshi Dr Ofweneke walitengana mapema mwaka 2017 baada ya kudumu pamoja kwa muda mrefu.

Ofweneke alikuja akakubali yalishamwagika na kumpata mwanamke mwingine huku pia Nicah akipata mwanaume mwingine ambaye ni DJ Slahver.

Nicah na Slahver wamekuwa pamoja kwa muda mrefu pia ambapo mapema mwaka hu wakati wa sikukuu ya Valentino, alipakia video akimuosha miguu mwanaume huyu – video ambayo iliibua mjadala, baadhi wakizua kuwa ni njama ya wanawake kuwapumbaza wanaume ili kuwanunulia zawadi za siku hiyo ya wapendanao duniani.

Kama mahusiano mengine mengi, wawili hao hawajapata mteremko katika uhusiano wao bali pia wamekosana mara kadhaa, mara ya mwisho Nicah alitangaza kutengana na Slahver.

Wiki chache baadae walirudiana tena mpaka sasa hivi ambapo wamefanikisha kuhamisho uhusiano wao kutoka kwa wapenzi hadi kwa wachumba na inshallah mashabiki wao watawaona wakifunga harusi na kuwa wanandoa.