Utabiri uliotimia? Video Ezekiel akionya kuhusu maisha magumu miezi 6 baada ya uchaguzi

"Mtachinjwa kiuchumi hadi mshangae. Na nimewaambia bila kuwalipisha na mubashara runingani. Mtalia na kuzunguka…” Ezekiel alisema.

Muhtasari

• Video hiyo ambayo imeibuliwa sasa inakisiwa kunaswa kipindi Uhuru Kenyatta anajiandaa kuondoka ofisini.

Mchungaji Ezekiel Odero wakati wa ibada ya Meza ya Bwana Jumamosi.
Mchungaji Ezekiel Odero wakati wa ibada ya Meza ya Bwana Jumamosi.
Image: MAKTABA

Kuna msemo maarufu ambao watu wanasema kwamba mitandao ya kijamii huwa haisahau jambo au tukio, mradi limepakiwa kule.

Msemo huu umeibua maana halisi na yenye mashiko mitandaoni baada ya watumizi wa mitandao hiyo kuibua video ambayo haijulikani ni ya lini ikimuonyesha mchungaji wa kanisa la NEew Life Prayer Centre kule Mavueni Kilifi Ezekiel Odero alizungumzia kile kilichoonekana kama ni utabiri kuhusu matukio ya humu nchini na ambayo wengi wanahisi kwamba utabiri huo umekuja kutokea kweli.

Odero katika video hiyo ambayo kwa muktadha wake inadhaniwa kunaswa kipindi cha kampeni kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka jana anaonekana akiwaonya Wakenya kuhusu uongozi ambao ungekuja, na kusema kuwa wengi wa wale waliokuwa wakimsuta rais mstaafu Uhuru Kenyatta wangefika muda na kuhisi kwamba alikuwa afadhali kidogo kuliko mrithi wake – na hili halimaanishi kwamba tunasema uongozi wa sasa umevurunda, la hasha!

Odero katika video hiyo anasikika akiwaonya watu haswa wa eneo la Mlima Kenya ambao hawakuwa wanamtaka Kenyatta, akisema kuwa watamkosa sana na kuona umuhimu wake baada ya kustaafu, lakini kwa bahati mbaya hatojitokeza kuwasaidia kwani hatakuwa na mamlaka tena.

“Rais Kenyatta alifunga mianya ya wizi lakini hakuna mtu anamtaka sasa hivi, ‘akwende’ mpaka watu wa Mlima Kenya hawamtaki rais Kenyatta. Mtachinjwa asubuhi. Siwadanganyi, nyinyi watu wa eneo la kati mliomkataa Uhuru Kenyatta mtachinjwa kiuchumi. Na nimewaambia bila kuwalipisha na mubashara runingani. Mtamlilia na kuzungukuka…” Odero anaonekana akitoa utabiri.

Mhubiri huyo ambaye kwa sasa anapitia mchakato wa kesi kuhusiana na mafunzo potovu kwenye kanisa lake la Mavueni alitoa mfano wa nyuma jinsi watu walimkataa hayati rais wa tatu Mwai Kibaki licha ya kufanya juhudi mpaka za kujenga barabara kuu ya Thika.

“Rais Kenyatta alipokuja kwa miaka kumi, Kenya mko na stima karibia wote, barabara ni safi, hospitali zimebadilika… haya nyang’au anakuja. Nawaahidi na niko hapa nchi hii na serikali inayokuja miezi sita mtasikia ile skendo itakuja na huyo atakayeweka hiyo serikali uongozini ni nyinyi….” Odero alisema kwa utabiri.

Hii hapa video yenyewe: