Amber Ray asimulia masaibu aliyopitia na baba wa mtoto wake wa kwanza

Mwanasosholaiti huyo alidokeza kuwa Rapudo kuja katika maisha yake na kupata mtoto naye ni baraka ya kweli.

Muhtasari

•Katika video ambayo alichapisha, Bw Rapudo alionekana akimuosha mtoto wao huku Amber Ray akiwa ametulia

•"Na baby daddy wangu Mkikuyu, hili lilikuwa mwiko 'ati hizo ni kazi za wanawake utamaduni hauruhusu," Amber alisema.

Image: INSTAGRAM// AMBER RAY

Mwanasosholaiti mashuhuri wa Kenya Faith Makau almaarufu Amber Ray amemshambulia baba ya mtoto wake wa kwanza, Baba Garvin huku akimmwagia sifa kemkem mpenzi wake wa sasa, Kennedy Rapudo.

Katika chapisho lake la Jumatatu, mama huyo wa watoto wawili alionyesha video ya Bw Rapudo akimsaidia na kazi za nyumbani. 

Huku akioneyesha kufurahishwa na kitendo cha mfanyibiashara huyo,  Amber Ray alionekana kumkosoa  mpenzi wake wa zamani akidai kwamba hilo ni jambo ambalo hangeweze kamwe kufanya.

"Na baby daddy wangu Mkikuyu, hili lilikuwa mwiko 'ati hizo ni kazi za wanawake utamaduni hauruhusu," Amber alisema.

Aliongeza "Na saa hizo hakuna kijakazi, maji nachota kwa kisima alafu naosha nguo (kwanza nepi), napika kisha nakaa macho usiku kucha nikimuangalia mtoto."

Mwanasosholaiti huyo alidokeza kuwa Rapudo kuja katika maisha yake na kupata mtoto naye ni baraka ya kweli.

"Watu wangu, hii ni moja ya maombi yangu yaliyojibiwa," Alisema.

Katika video ambayo alichapisha, Bw Rapudo alionekana akimuosha mtoto wao huku Amber Ray akiwa ametulia. Wapenzi na wazazi wenza hao walionekana kuwa ndani ya chumba cha mtoto wao mchanga.

Amber Ray na Kennedy Rapudo walitangaza kuzaliwa kwa mtoto wao wa kwanza pamoja mwezi.

Mwanasosholaiti huyo alishiriki habari hizo njema kwenye mitandao ya kijamii akimkaribisha mtoto wao wa kike ulimwenguni.

"Kuhusu msemo 'unaishi mara moja tu" Ninaanza kujiuliza jinsi hiyo ni kweli! Je, inaweza kuwa kweli kwamba siku moja ni kama miaka elfu na miaka elfu kama siku? Ninaweza kuwa na maswali machache zaidi ambayo hayajajibiwa, lakini kwa sasa...

"Mtu wangu yuko pamoja nami kama malaika wa nyumba yangu na mimi ni mama mpya kabisa! Karibu nyumbani mtoto A...nimekuhisi maisha haya yote na sasa naweza kukuona, kukusikia, na kukugusa...NI MAISHA MPYA KABISA 🙌🏾 Maisha ya maisha mengi," Amber Ray aliandika.

Wakati huo huo, Rapudo pia aliweka picha za mpenzi huyo wake akiwa hospitalini baada ya kumkaribisha mtoto wao.