"Wambea kimewaramba!" Amber Ray na Rapudo waotesha upya mapenzi yao

Wawili hao walionekana katika mfululizo wa picha za pamoja, wiki tatu tu baada ya kudai kutengana.

Muhtasari

• “Kuongelelea mambo ya watu wawili wamelala ndani ya blanket moja nisijikute........... nimebaki na matope,” huyu alisema.

Kennedy Rapudo na mpenzi wake Amber Ray
Kennedy Rapudo na mpenzi wake Amber Ray
Image: Instagram

Wambea na mashemeji wa mitandao ya kijamii wamebaki na makoko usoni baada ya mwanasosholaiti Amber Ray na aliyekuwa mpenzi wake Kennedy Rapudo kurudiana.

Amber Ray alipakia mfululizo wa picha za pamoja katika mwendelezo wa video akimtakia Rapudo kheir njema ya siku ya kuzaliwa, hivyo kufutilia mbali uvumi wa kuachana ambao waliuanzisha wenyewe.

Wiki tatu zilizopita, mber Ray na Rapudo walitupiana maneno kwa njia za mafumbo mitandaoni huku kila mmoja akizifuta picha za mwenzake mitandaoni.

Katika kudhibitisha kuvunjika kwa uhusiano wao, Rapudo alidokeza kuwa alikuwa anasubiria miezi miwili tu mtoto azaliwe ili wabaini mbivu na mbichi kama ndiye baba.

Ray alimjibu vikali akisema kwamba safari hii hatoweza kukaa kimya ex wake akimchafulia jina kwani imekuwa mazoea ya wapenzi wake wa zamani pindi tu wanapoachana wanaanza kumchafulia jina ili aonekane yeye ndio mbaya.

Ray alisema kuwa safari hii atasimama kidete na kupambania jina lake hadi mwisho wa Dahari.

Lakini kurudiana kwao kumewaacha na tope usoni wale ambao waliingilia ugomvi wao, wengine wakimshauri Ray kutomrudia Rapudo na badala yake kuzingatia afya ya mimba yake.

“Wakenya wambea kimewaramba,” mmoja aliwasuta waliokuwa wakiingilia ugomvi wa wapenzi hao.

“Naanza kujifunza jinsi ya kujali mambo yangu tu, ya watu siwezi tena😂🤣💔        😭”

Kuongelelea mambo ya watu wawili wamelala ndani ya blanket moja nisijikute........... nimebaki na matope,” huyu alisema.

Hata hivyo, baadhi walisema kuwa walijua ni kiki tu za mitandaoni lakini kiuhalisia walikuwa bado paoja tu.

“Mimi ndiye mtu pekee niliyeamini kuwa watu bado mko pamoja 💯 happy birthday 🎂 kwake,” alisema mwingine.