Pritty Vishy aonyesha umbo lake huku akiwatia moyo wanawake wenye mwili kama wake kukumbatia miili yao

Vishy alieleza kuwa anawatia moyo wanawake wenye saizi kubwa kukumbatia miili yao.

Muhtasari

• Pritty Vishy alipakia kwenye ukurasa wake wa Instagram video yake akionyesha umbo lake akiwa pwani kule Mombasa. 

• Video hiyo ilizua gumzo mtandaoni baina ya mashabiki katika sehemu ya maoni kwani mashabiki wengi walimrushia cheche za matusi huku wengine wakimpongeza kwa umbo lake na kwa ujasiri aliokuwa nao.

Pritty Vishy aonyesha umbo lake na kuwahimiza wanawake wenye miili kubwa kukumbatia miili yao.
Pritty Vishy aonyesha umbo lake na kuwahimiza wanawake wenye miili kubwa kukumbatia miili yao.
Image: Instagram

Aliyekuwa mpenzi wa rapa Stivo Simple Boy, Pritty Vishy alipakia kwenye ukurasa wake wa Instagram video yake akionyesha umbo lake akiwa pwani kule Mombasa.

Vishy, kwenye chapisho katika ukurasa wake wa Instagram, alieleza kuwa anawatia moyo wanawake wenye saizi kubwa kukumbatia miili yao.

"Nauza kujiamini kwa malkia wangu wenye miili kubwa zaidi😂," mpenzi huyo wa sasa wa Dj_starvy aliandika.

Video hiyo ilizua gumzo mtandaoni baina ya mashabiki katika sehemu ya maoni kwani mashabiki wengi walimrushia cheche za matusi huku wengine wakimpongeza kwa umbo lake na kwa ujasiri aliokuwa nao.

"Tumbo inafanya nini kwa suruali😮," terry_wanjiru_ aliulizia huku  huku akimtania.

"Hapa uneza tafta rosecoco na torch 😂😂😂," official_ballitra aliandika huku akimalizia na emooji za kicheko.

"we ni mrembo bila mwili😮," Way_lay._  aliandika.

"Hutaki kunitag kwa sababu hutaki niwe mshikaji😮😮😢," mpenzi wake Vishy, Dj starvy aliandika kwa mbwembwe.

"Mabao ya mwili milayaaaaa 😍😍," aliandika Chokuu kwa mbwembwe.

"😍😍😍😍you pretty girl... mwenyewe anasema zimelala aende aangalie za mamake kama zimesimama Bado .. kama matiti were meant kusimama zingeumbwa na mfupa..mm," Kimfaymah aliandika.