Kutana na mpenzi wa kwanza wa Akothee

Alisema kuwa ni yeye aliyeunyakua “Virginity” yake

Muhtasari

•Inaaminiwa kuwa, wakati huo aliuchukua ubikira wake, mbali na kumpa mabinti warembo watatu.

•Akothee pia alieleza kuwa, huyo ndiye mwanaume aliyemfunza kuwa watu hupeana busu huku akieleza kuwa alitoroka na midomo yake huku akishangaa kwa nini ayale mate ya mwingine.

Image: Facebook// Akothee

Takribani miaka minne iliyopita, Akothee aliposti mwanaume wa kwanza kusuhubiana naye kimapenzi.

Inaaminiwa kuwa, wakati huo aliuchukua ubikira wake, mbali na kumpa mabinti warembo watatu.

Katika ukurasa wake wa Facebook, Akothee aliposti, “ See my first love, the man who broke my virginity, the father of my 3 beautiful daughters.” Ambayo katika tafsiri, Mwone mpenzi wangu wa kwanza, aliyeuvunja ubikira wangu, baba wa wasichana wangu watatu warembo.

Akothee pia alieleza kuwa, huyo ndiye mwanaume aliyemfunza kuwa watu hupeana busu huku akieleza kuwa alitoroka na mdomo wake huku akishangaa kwa nini ayale mate ya mwingine.“ I always ran away with my mouth, wondering why should I eat somebody’s saliva; Nilikimbia na mdomo wangu huku nikishangaa kwa nini nile mate ya mwingine.

Aliendelea kusimulia kuwa, licha ya kutengana naye, waliyapitia mengi pamoja hadi wakati wazazi wake walimkataa bado alisimama naye. Licha ya kuwa mwanafunzi, wakati wazazi wake wakimfurusha alihakikisha kuwa ameandamana naye.

Esther Akoth maarufu Akothee pia alidakia mpenzi wake alipokuwa mwanafunzi katika chuo kikuu cha Moi, alimpa shilingi 3000, wakati wa kufunguliwa kwa shule jambo ambalo lilimfurahisha sana.

Alisimulia namna alivyoanza biashara yake katika kibanda kidogo cha matunda, na kunawiri hadi kuwa duka kubwa, yote kwa hisani ya mpenzi wake huyo.“ I could not fit in my mothers house anymore with a hand of children, I grew wings I had to fly, RESPECT MAN JARO, my grocery grew  and i rented a shop, then I extended my business into selling cloths.” Alieleza; ambayo tafsiri yake;Singetoshea zaidi katika nyumba ya mamangu, niliota mabawa nikapuruka maana pia nilikuwa na watoto. Kibanda changu kilikua hadi nikakodisha duka nikaanza kuuza nguo. HISANI YA MWANAUME JARO.

Akothee pia alisema kuwa, baada ya kujimudu kidogo katika maisha alirudi kusoma kwa kuwa hiyo ndiyo ilikuwa ndoto ya mamake mzazi, akisema kuwa, mpenziwe Jared anafaa kuheshimiwa. Jared, mume wa kwanza wa Akothee ana shahada ya uzamili, amejikimu kifamilia.