USHAURI KWA KINA MAMA

Akothee awashauri wanawake wenzake waache kushindana

Tumia nguvu hiyo kujiinua mwenyewe, huwezi vunja kile ambacho hukujenga.

Muhtasari

•Usione mwanamke yeyote kama shindano lako.Hii ndio sababu pekee wanawake hawasaidii wanawake wenzao.Kama mwanamke, wakati utahisi kumwangusha mwanamke mwenzako, elewa uko chini yake tayari na ndiyo sababu pia unataka kumwangusha awe katika kiwango chako.

•Haya yanajiri wakati ambapo alimtumia ujumbe mtamu wa kumtia moyo rafiki yake Azziad liyekuwa akisherehekea anasherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Mwanamuziki Esther Akoth maarufu Akothee ametoa wito kwa wanawake kuwa waache kuchukiana na badala yake kushauriana na kuinuana.

Akothee katika mtandao wake wa Instagram alisema kuwa, wanawake wasione mwanamke yeyote kama wanashindana. Alisema kuwa wakati mwanamke ataanza kuhisi kumwangusha mwanamke mwenzake, atakuwa anajiangusha mwenyewe.

“Never see any woman as your competition,that's the only reason women don't support other women. As A woman ,the moment you feel like bringing another woman down ,just understand that you are already below her and that's why you want her to drop down to your level” Aliposti.

Usione mwanamke yeyote kama shindano lako.Hii ndio sababu pekee wanawake hawasaidii wanawake wenzao.Kama mwanamke, wakati utahisi kumwangusha mwanamke mwenzako, elewa uko chini yake tayari na ndiyo sababu pia unataka kumwangusha awe katika kiwango chako.

Akothee aliendelea kuwashauri kuwa, badala ya kufanya  hivyo wangetumia nguvu hiyo kujiimarisha kwani hawawezi bomoa kile ambacho hawakujenga.“Use that energy to empower yourself,you can't break what you didn't build. Some people were ment to succeed through your negativity,it's a way God use you to propel them to their final destination called SUCCESS.” Aliongeza

Tumia nguvu hiyo kujiinua mwenyewe, huwezi vunja kile ambacho hukujenga. Watu wangine waliumbwa kupata ufanisi kutokana na ubaya wako, ndiyo njia Mungu hutumia kuwapeperusha hadi kwa hatua ya mwisho katika safari, inayojulikana kama ufanisi.

Haya yanajiri wakati ambapo alimtumia ujumbe mtamu wa kumtia moyo rafiki yake Azziad liyekuwa akisherehekea anasherehekea siku yake ya kuzaliwa.