Mwanamume avalia sodo, adai ndio njia ya kuleta joto kwenye korodani

Mbinu hii yake ya kuweka korodani zake joto kwa kuvaa sodo si ya kawaida hivyo basi, ilizua hisia mseto mtandaoni.

Muhtasari

• Mtumizi wa Twitter anayejulikana kama KingDon_za alipakia picha mnamo siku ya Jumanne, Julai 4, akionyesha sodo hizo ndani ya chupi yake huku akifichua kwa nini anazivaa. 

Mwanamume avaa sodo ili kuweka korodani yake joto na adai kuwa anahisi raha.
KingDon_Za Mwanamume avaa sodo ili kuweka korodani yake joto na adai kuwa anahisi raha.
Image: Twitter

Mwanamume mmoja amezua gumzo kwenye Twitter baada ya kufichua kuwa anavaa sodo ili kuziweka korodani zake joto.

Mtumizi wa Twitter anayejulikana kama KingDon_za alipakia picha mnamo siku ya Jumanne, Julai 4, akionyesha sodo hizo ndani ya chupi yake huku akifichua kwa nini anazivaa.

Jamaa huyo alisema sodo hizo humpa joto na kuwataka wanaume wenzake kuiga mfano huo.

"Nimekuwa nikivaa sodo ili kuweka korodani zangu joto, bidhaa hizi ni nzuri. Kuvaa hizi kila siku ni faafu 10/10," KingDon_Za aliandika.

Mbinu hii yake ya kuweka korodani zake joto kwa kuvaa sodo si ya kawaida hivyo basi, ilizua  hisia mseto mtandaoni.

Wanamitandao wengi walionyesha kutofurahishwa na chapisho hilo ,kwani wengi wao walidai kuwa wangependa korodani zao kuwa baridi huku wachache wakionyesha kufurahishwa na kudai kuwa watajaribu.

Baadhi ya maoni hayo ni kama yafuatayo.

"Korodani joto hufanya nini yenye korodani baridi haiwezi???" Tonnie_Ntogo aliuliza.

"Lol... sodo ni bei ghali," Freanky4fingers aliandika.

"Kwa nini ulinunua chupi ya njano?" VinDollar016 aliuliza.

"Nitajaribu ili kuhakikisha kama unachosema ni sawa..."OnlyaBeing aliandika kwa mbwembwe.

"Ni afadhali wapate baridi na kusinyaa. Siwezivaa sodo,” Sbugelo aliandika.

"Kwa hivyo wazee wetu walivaa suruali kubwa zilizolegea, chupi ya wanaume ikiwezekana suruali fupi isiyobana sana. Usipike mayai hayo 🍳 wewe bado mchanga," Dipruz alishauri.

 "Ulimwengu unakaribia mwisho, aibu," JackzMind alisema.