Pesa ni kitu bure kabisa unaweza kuwa nayo - Dr. Ofweneke

"Kati ya vitu vyote watu wanaweza miliki maishani, pesa ni kitu kisicho na maana kabisa.” Dr. Ofweneke alisema.

Muhtasari

• Mcheshi huyo alihoji kuwa pesa si kitu cha maana kwake na kuwa pesa anazopokea ilikuwa kama ishara shukurani tu.

• Baba huyo wa watoto wawili alifutilia mbali tetesi kuwa kulikuwa na mahusiano zaidi ya mahusiano ya kikazi baina yake na mtangazaji mwenza wa kipindi cha MR.Right, Diana Bahati.

Dr Ofweneke asema Akothee alimpa 1.4m kuwa MC wa harusi yake.
Dr Ofweneke asema Akothee alimpa 1.4m kuwa MC wa harusi yake.
Image: Instagram

Mchekeshaji Dr. Ofweneke amekiri kuwa hatambui pesa katika maisha yake akiongeza kuwa kwake pesa ni kitu kitu kisicho na maana kabisa.

Dr. Ofweneke alisema haya akiwahutubia wanahabari baada ya kuzinduliwa kama balozi wa pombe ya Glendale.

“Kwangu si pesa, kwa namna yoyote ile sipendi pesa mimi. kati ya vitu vyote watu wanaweza miliki maishani, pesa ni kitu kisicho na maana kabisa.”

Mcheshi huyo alihoji kuwa pesa alizopokea kutoka kwa dili hiyo ilikuwa kama njia ya kampuni hiyo kumshukuru tu na hakuhitaji pesa hizo kwa njia yoyote ile.

“Siezi fanya kazi hii kwa bure kwa sababu nina watoto katika za kifahari na mke mrembo ninayehitajika kummaintain. Lakini wacha niweke wazi mjue kile ambacho nalipwa hapa ni ishara ya shukrani.”

Baba huyo wa watoto wawili alifutilia mbali tetesi kuwa kulikuwa na mahusiano zaidi ya mahusiano ya kikazi baina yake na mtangazaji mwenza wa kipindi cha MR.Right, Diana Bahati. Aliwaomba wanahabari kuwa na keshima kwa ndoa yake.

“Asheni kamera zenu, kuna taarifa nataka niwaambie. Ndio kuna mahusiano kati yangu na Diana Bahati, tunafanya kazi pamoja na hilo ndilo linaloendela kati yetu.”

Miezi miwli iliyopita, Startimes walizindua msimu wa tatu wa kipindi cha Hello Mr Right kinachongozwa na mchekeshaji Dr Ofweneke na msanii Diana Marua..

Katika uzinduzi wa kipindi hicho cha kuchumbiana, mumewe Diana Marua, Bahati Kioko alionesha wasiwasi wake kuhusu kazi hiyo mpya ya mkewe, akionekana kuingiwa na mashaka kuwa huenda mengine yakatokea katika mazungumzo kuhusu suala zima la kuchumbiana.

“Tafadhai, mimi sijakuja kukusapoti, hata sijakuja kuona uzinduzi, nimekuja tu kuona vile unakaribiana na mke wangu. Huko kukaribiana chunga sana eeh,” Bahati alimwambia Dr Ofweneke.

Katika uzinduzi huo Ofweneke alijivunia ubalozi huo na kampuni hiyo ya pombe kwa sababu kwake alihisi pombe hiyo ilikuwa ya kifahari sana na yeye mwenye anafahamika kwa sababu ya hadhi yake katika jamii.