Wanandoa wamuuza mwanao wa miezi 8 ili kununua iPhone 14 kwa ajili ya Reels Instagram

Si mara ya kwanza kwa wapenzi hao kujaribu mbini za kutafuta iPhone kwa udi na uvumbi kwani iliripotiwa mara ya kwanza walijaribu kumuuza mwanao wa miaka 7 lakini hawakupata mnunuzi.

Muhtasari

Mtoto wao alitoweka kwa siku kadhaa na wnandoa hao hawakuonesha wasiwasi wa kumtafuta, jambo lililowafanya majirani kuhisi kuna njama.

Walipomkabili mama, alikiri kwamba walimuuza ili kupata simu ya kifahari aina ya iPhone 14.

Image: BBC

Kisa cha kusikitisha kimeripotiwa katika jimbo la Bengal nchini India ambapo wanandoa wameripotiwa kumpiga mnada mwanao wa siku 18 tu ili kupata pesa za kununua simu aina ya IPhone kwa ajili ya kujivinjari katika mitandao ya kijamii.

Kwa mujibu wa jarida la Indian Times, Polisi wa Bengal Magharibi walifanikiwa kumkamata mama huyo aliyetambulika kwa jina la 'Sathi' ambaye alihusika kununua?? au kuuza?? mtoto. Walakini, baba, Jaydev Ghosh, bado yuko mafichoni, na viongozi wanamtafuta kwa bidii.

Tukio hilo lilikuja kujulikana wakati majirani waliohusika waligundua mabadiliko fulani ya kipekee katika tabia ya familia ya Ghosh.

Mtoto huyo wa miezi minane alikuwa ametoweka kwa siku nyingi, lakini wazazi hawakuonyesha dalili zozote za wasiwasi au mashaka.

Zaidi ya hayo, ununuzi wao wa ghafla wa iPhone 14, ambao gharama yake si chini ya laki moja, ulizua shaka miongoni mwa majirani, ikizingatiwa kuwa familia hiyo ilijulikana kuwa na matatizo ya kifedha hapo awali.

Majirani walipomkabili mama huyo, hatimaye alikiri chini ya shinikizo kwamba yeye na mumewe walikuwa wamemuuza mtoto wao ili kupata pesa za kununua iPhone, na kuwawezesha kuunda reels za Instagram zinazoonyesha safari zao katika sehemu mbalimbali za Bengal.

Jambo la kushangaza hata zaidi, ilifichuliwa kwamba kabla ya kujaribu kumuuza mtoto wao mchanga, baba huyo pia alikuwa amejaribu kumuuza binti yake wa miaka saba.

Polisi wamefungua kesi dhidi ya wanandoa hao, na mama aliyemnunua mtoto huyo pia anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu wa kusafirisha binadamu.

Uchunguzi bado unaendelea, na maelezo zaidi yatatolewa mara tu polisi watakapochunguza kwa kina kesi hiyo.