Davido ajibu ombi la mjakazi wake kwa kumnunulia zawadi ya simu ya Iphone 14 pro max

Kwa mshangao Davido aliandika ‘nilijibu maombi yake’ kwa kumpa simu mpya kabisa aina ya iPhone 14.

Muhtasari

• Baadaye iligundulika kuwa mfanyakazi huyo wa nyumbani alikuwa amelalamika kwa mtu mashuhuri wa Nigeria kwamba alihitaji simu mpya.

Davido adaiwa kumzawidi mjakazi wake simu ya Iphone,
Davido adaiwa kumzawidi mjakazi wake simu ya Iphone,
Image: Instagram//GossipMillTV

Davido anasifika kwa ukarimu wake, na alidhihirisha hilo kwa mara nyingine tena alipompa mjakazi wake zawadi ya simu aina ya iPhone 14 Pro Max.

Baadaye iligundulika kuwa mfanyakazi huyo wa nyumbani alikuwa amelalamika kwa mtu mashuhuri wa Nigeria kwamba alihitaji simu mpya.

Kwa mshangao Davido aliandika ‘nilijibu maombi yake’ kwa kumpa simu mpya kabisa aina ya iPhone 14. Msafishaji huyo alimsifu OBO kwenye video ambayo imesambaa mitandaoni na kuomba Mungu ambariki sana.

Zaidi ya hayo, alidai kutumia kifaa cha Android, akionyesha kwamba hii ni mara yake ya kwanza kutumia bidhaa ya Apple - ya kifahari na ya gharama kubwa.

Davido alikuwa kwenye habari hivi majuzi alipofichua kwa nadra kuhusu Aliko Dangote, mtu tajiri zaidi barani Afrika. Alidai kuwa licha ya utajiri mkubwa wa Dangote, yeye hununua magari mawili pekee kila baada ya miaka minane.

Muigizaji huyo wa Nigeria alifichua hayo katika mahojiano ya hivi karibuni na Forbes, ambapo pia alitaja kuwa milionea huyo anampa ushauri wa kifedha.

Mwanamuziki huyo ambaye hivi majuzi alitumbuiza kwenye Tamasha la Timeless, Jumapili, Aprili 23, 2023, jijini Lagos pia alidai kuwa Dangote huwa anamshauri kuhifadhi fedha zake na kujiepusha na matumizi makubwa.

Davido alisema; “Mjomba Aliko ni bilionea wa aina tofauti sana. Mjomba Aliko hununua kama magari mawili kila baada ya miaka minane. Ni bilionea mwenye nidhamu na tofauti sana. Kila ninapomwona anasema jambo moja tu, ‘Hifadhi pesa zako!’. Hakuna zaidi ananiambia, kila wakati weka pesa zako. Yeye na baba yangu wamekuwa marafiki wa karibu sana.”

Kumzawadi mfanyikazi wake wa nyumbani na simu kunakuja siku moja tu baada ya habari kuzagaa kwamba msanii huyo alijinunulia gari la kifahari la Maybach Virgil Abloh la 2023 ambalo linadaiwa kuenda kwa takribani milioni 117 za Kenya.

Gari hilo lina upekee uliotukuka kwani ni moja kati ya magari 150 tu ya Maybach 2023 ambayo kampuni husika iliunda.

Baadaye, inasemekana alitumia $400,000 zaidi kwenye saa ya Patek Philippe ili kukamilisha ununuzi wake wa hivi karibuni wa kifahari.