Arrow Bwoy akubali Nadia sio mkewe,aomba msaada wa pesa kulipa mahari yake

Aliendelea kuwasihi Wakenya kumsaidia kuchangisha mahari ili apate mke kwa njia ifaayo.

Muhtasari
  • Hii ni baada ya mchumba wake Nadia Mukami kuweka wazi kuwa hajichukulii kuwa mwanamke aliyeolewa.
  • Kwenye mahojiano ya Kiss FM na Chito na Kwambox, msanii huyo alisema hadi Arrow atampeleka njiani na kumlipia mahari hatajiona amechukuliwa.
Nadia Mukami na Arrow Bwoy
Image: HISANI

Mkurugenzi Mtendaji wa Utembe Arrow Bwoy yuko nje akiomba Wakenya usaidizi wa kifedha ili kuweza kumlipia mahari Nadia Mukami.

Hii ni baada ya mchumba wake Nadia Mukami kuweka wazi kuwa hajichukulii kuwa mwanamke aliyeolewa.

Kwenye mahojiano ya Kiss FM na Chito na Kwambox, msanii huyo alisema hadi Arrow atampeleka njiani na kumlipia mahari hatajiona amechukuliwa.

Ingawa Arrow alikuwa amependekeza Mukami mnamo Machi 2022, anasema bado hajachukua hatua zaidi na kumlipa mahari.

"Sijaolewa. Ni ukweli. Hajalipa mahari yangu. Yuko nami kwa mkopo," alifichua haya wakati wa mahojiano Ijumaa.

Nadia alimwaya mtama na kusema;

"Niko soko, mimi ni mpenzi wako tu. Sio mke. Anitoe soko rasmi."

Aliendelea kusema;

"Ukitaka niseme nimeolewa, Unajua anuani ya mzazi wangu, mahari yangu kama bibi ambaye ni msomi sana ni ya juu sana na mimi ni Nadia Mukami kwa hivyo bado iko juu,".

Katika kujibu kwa haraka, Arrow Bwoy alikiri kwamba hana mke bado kwa sababu ya kushindwa kulipa mahari.

Aliendelea kuwasihi Wakenya kumsaidia kuchangisha mahari ili apate mke kwa njia ifaayo.

“Ni ukweli sina wife juu sijafikisha pesa ya Mahari. Nomba mnichangie tafadhali. Tunma kwa Number yake 0704403403 @ChrisKirwa aki sort mambo ya pay bill,” Arrow Bwoy alisema.

Wawili hao wamebarikiwa na mtoto mmoja,huku wakiwa pamoja kama wapenzi kwa muda.