Mwanaume alia akikodisha nyumba ya starehe baada ya kuishi mitaani kwa miaka mingi (Video)

Katika video hiyo, anaonekana akipiga magoti kwenye sakafu ya makao yake mapya, akiwa amejawa na hisia anapotafakari safari yake kutoka kwa ukosefu wa makao hadi mahali pa faraja na usalama.

Muhtasari

• "Kutoka kwa kuishi mtaani hadi mahali pazuri sasa (hadithi ya kweli ya maisha). Huyo Mungu aliyenitembelea, atakuona, Sema amina.”

Jamaa akilia.
Jamaa akilia.
Image: TikTok

Mwanamume mmoja katika mtandao wa TikTok amewashangaza wengi baada ya kupakia video akilia macozi ya furaha huku akijigaragaza kwenye zulia sakafuni.

Mwanamume huyo alihadithia kwamba sababu ya kulia kwake ilikuwa ni mara yake ya kwanza kukodisha na kuishi kwenye chumba chenye hadhi nzuri, baada ya kuishi mitaani kwa miaka mingi ya maisha yake.

Katika video hiyo, anaonekana akipiga magoti kwenye sakafu ya makao yake mapya, akiwa amejawa na hisia anapotafakari safari yake kutoka kwa ukosefu wa makao hadi mahali pa faraja na usalama.

Aliandika;

"Kutoka kwa kuishi mtaani hadi mahali pazuri sasa (hadithi ya kweli ya maisha). Huyo Mungu aliyenitembelea, atakuona, Sema amina.”

Maoni ya Wanamtandao...

@chiomsy alijibu; "Kuanzia kuchuchumaa na watu hadi kumiliki nafasi yangu mwenyewe mtu huyo mbinguni hajawahi kunikosa dada."

@QueenJuliet alijibu; "Sikulii, ninajaribu tu kusema pongezi."

@Darkskin_Didi alisema; "Sijui lakini ni thabiti."

 

@laeti alitoa maoni; "Ameen mungu mwenye uwezo atanifanyia mimi pia d."

 

@Jenny AY alijibu: "Hongera."

 

@Abraham Praise alisema; “Ninapata baraka zako naomba uende unipe ushuhuda wangu pia.”

 

@Loemashs alijibu; "Mungu ni thabiti sana."

 

@Deran alijibu; “Hongera sana.”