YouTube yafunga akaunti ya Mwanablogu Andrew Kibe

Andrew Kibe ameghadhabishwa na hatua za Youtube kusimamisha kurasa zake za Youtube.

Muhtasari

•Andrew Kibe amelazimika kufanya mabadiliko  makubwa baada ya kurasa wake wa Youtube wenye  mashabiki zidi ya  elifu mia inne (400 K) wanaommfuatilia kufungwa .

•Aliweka wazi kuwa haungi mkono hatua zilizochukuliwa na mtandao huo dhidi yake, 

Muunda maudhui wa Marekani, Andrew Kibe.
Muunda maudhui wa Marekani, Andrew Kibe.
Image: INSTAGRAM

Mwana  blogu Andrew Kibe amelazimika kufanya mabadiliko  makubwa baada ya kurasa wake wa Youtube wenye  mashabiki zaidi ya  laki nne wanaommfuatilia kufungwa.

Japo Kibe hakueleza sababu zilizopelekea akaunti yake kufungwa, alitoa maelezo kuhusu hatua hiyo ya Youtube kwa mashabiki wake.

Aliwarai mashabiki wake wawe wenye subira na waaminifu kwani kuna jukwaa jipya ambalo maudhui yake yatatiririshwa.

Aliweka wazi kuwa haungi mkono hatua zilizochukuliwa na mtandao huo dhidi yake, ila alisema ana matumaini kuwa atarejea mtandaoni kwa njia zozote zile.

Katika ujumbe aliochapisha kwenye kurasa zake alisema;

"Nipate usiku wa leo kwenye, X, Rumble,Instagram, na Tiktok."

Mashabiki wake walishangazwa kuona kwamba kurasa za Andrew kibe zimesimamishwa kufuatia madai ya kukiuka kanuni na masharti ya mtandao huo.

"Akaunti ya Youtube inayohusishwa na video hii imesitishwa,"

Awali Kibe alikua amchapisha video kwenye mitandao akimkmea vikali kijana mmoja  mfanyibiashara ambaye alilazimia kufunga biashara zake za kuuza mayai ya kuchemshwa ili kuendelea na masomo yake, jambo ambalo Kibe alilichukulia kuwa ni la kupoteza muda.

Kulingana na sheria za Google zenye uwezo wa kusimamisha akaunti zinasema kuwa;

Iwapo kituo chako kilikatishwa kwa sababu ya madai ya  ukiukaji wa hatimiliki na unahisi madai hayo si sahihi, unaweza kuwasilisha arafa ya kukanusha. Ila fomu ya wavuti ya arafa ya kukanusha haitapatikana.

Hili linatia shaka kwa mwanablogu huyo kwani Youtube inaweza kusimamisha akaunti kwa muda au kabisa.

Kibe amejibu madai haya katika ukurasa wake wa Tiktok akisema kuwa bado angali imara kwa kazi zake na kuhakiki kuwa hatua zilizochukuliwa hazitamzuia kutoa huduma zake.

Cha kutia moyo kwa Mwanablogu huyu sasa ni kuwa, mashabiki wameahidi kumfuata katika mtandao wowote ule ili kupata huduma zake.