Kina baba wenye mabinti huishi miaka mingi kuliko kina baba wenye wavulana - utafiti

Idadi ya mabinti ilihusiana vyema na muda mrefu wa maisha ya baba zao, na kuongeza maisha yao marefu kwa wastani kwa wiki 74 kwa kila binti aliyezaliwa.

Muhtasari

• Kinyume chake, kwa wanawake, idadi ya mabinti na idadi ya watoto wa kiume ilipunguza maisha marefu ya uzazi.

Baba na bintiye
Baba na bintiye
Image: BBC NEWS

Utafiti wa hivi karibuni unaonesha kwamba jinsia ya mtoto ambayo mtu huzaa inachangia pakubwa katika muda wake wa kuishi humu duniani.

Kwa mujibu wa utafiti huo uliofanywa na wakfu wa National Library Medicine, wanadai kwamba kina baba wenye mabinti huishi kwa miaka mingi Zaidi duniani ikilinganishwa na kina baba wenye watoto wa kiume au mseto wa wavulana na wasichana.

Utafiti huo ulifichua kwamba uzazi na hali ya mtu ya kisaikolojia ni ghali sana, na mtu binafsi akiwekeza rasilimali katika kuzaa watoto anapaswa kuteseka na gharama kama vile kuzorota kwa hali ya afya na labda maisha mafupi.

Kwa kuwa mahitaji ya nguvu na lishe ya ujauzito na kunyonyesha hutoa gharama za uzazi juu zaidi kwa wanawake kuliko wanaume, wanawake wenye idadi kubwa ya watoto wanapaswa kuonyesha dalili za kuzorota kwa hali, wakati wanaume wenye familia kubwa hawapaswi, utafiti huo ulisema.

“Hata hivyo, ikiwa gharama za uzazi hupunguza maisha ya muda mrefu kwa wanawake bado ni ya shaka, na kwa wanaume suala hili halijashughulikiwa vya kutosha. Kwa kuongeza, kwa kuwa watoto wa kiume ni ghali zaidi kuzalisha kuliko binti, kuwa na watoto wa kiume kunapaswa kuwa na athari mbaya zaidi kwa maisha marefu ya uzazi kuliko kuwa na binti,” National Library Medicine walitafiti.

Kwa mujibu wa utafiti huo uliofanyika nchini Poland, wanaume waliokiri kuwa na watoto mabinti waliishi miaka mingi ikilinganishwa na wenzao wenye watoto wa kiume.

“Tunaonyesha kwa mara ya kwanza kwamba idadi ya mabinti ilihusiana vyema na muda mrefu wa maisha ya baba zao, na kuongeza maisha yao marefu kwa wastani kwa wiki 74 kwa kila binti aliyezaliwa, wakati idadi ya watoto wa kiume haikuwa na athari kubwa kwa maisha marefu ya baba,” walibaini.

Kinyume chake, kwa wanawake, idadi ya mabinti na idadi ya watoto wa kiume ilipunguza maisha marefu ya uzazi na kufanya hivyo kwa kiwango sawa, kwa wastani kwa wiki 95 kwa kila mtoto wa kiume au wa kike, ikionyesha kuwa kwa wanawake, gharama za kupata watoto wa kiume na wa kike zinafanana.

https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/16634019/