Nilifanya muziki kwa ukaidi wangu babangu hakutaka niwe mwanamziki Khadija Kopa asema

Khadija Kopa aliwashauri wazazi kuwaunga wanao mkono kuendeleza vipawa vyao.

Muhtasari

• Nilipenda muziki sana jambo ambalo lilifanya nikaidi amri ya baba, kwa sababu nilidhani muziki ndio kipawa changu.

Khadija Kopa
Khadija Kopa
Image: Hisani

Khadija Omari Kopa mwimbaji wa muziki wa Taarab na mtunzi wa nyimbo kutoka nchini Tanzania amezungumzia ziara yake katika tasnai ya muziki.

Khadija Kopa ambaye pia ni mamake mzazi msanii maarufu wa Bongo Zuchu amezungumzia swala la wazazi kukuza vipawa vya watoto wao akisimulia jinsi ambavyo babake alikataa taaluma yake ya kuwa mwanamuziki.

Nilipenda muziki sana jambo ambalo lilifanya nikaidi amri ya baba, kwa sababu nilidhani muziki ndio kipawa changu .

"Babangu mzazi hakutaka niwe mwanamuziki nilifanya muziki kwa ukaidi wangu alidhani nikifanya muziki nitapotoka kimaadili, ila kwangu muziki ni kipawa  nilizaliwa nacho, nilitaka kufanya jambo ambalo lingenifurahisha kwa maisha yangu yote ndio maana leo wengi wanaiga mfano wangu katika utunzi wa nyimbo",alisema.

Nyota huyo wa taarab aliwashauri wazazi kuwaunga wanao mkono kuendeleza vipawa vyao badala ya kuwa vizuizi kwa ndoto za wanao. 

"Watoto wapewe haki ya kujichagulia taaluma wanazopenda kutoka kwa nafsi zao ila wazazi wawape ushauri wa kutosha ndiposa wawe na maadili mema ndio wawe na mfano wa kuigwa na wengine, kipawa cha mtu ndio mafaniko ya maisha",alisema.

Khadija Kopa alisimulia kuwa  licha ya bintiye  Zuchu kusoma Diploma  katika  chuo kimoja nchini India wakati ulipofika wa kujiunga na chuo kikuu nchini China mwanaye alitaka kuanza taaluma yake ya  uwanamuziki jambo  ambalo Khadija Kopa alisema kuwa alikumbaliana nayo na kumpa  ushauri wa kutosha.