Zuchu hana mchumba yeyote, mwenye ako tayari alete mahari -Khadhija Kopa

Binti yangu hajaposwa hakuna yeyote amemlipia Mahari wengi kwenye mitandao wanasema Diamond ndio mpenzie.

Muhtasari

• Khadija Kopa alisema Diamond si mchumba wa Zuchu kwani hajaleta mahari wala hajamuoa kwa hivo mtu mwingine yeyote anaweza kuleta pesa zake za mahari.

Khadija Kopa na Bintiye Zuchu
Khadija Kopa na Bintiye Zuchu
Image: HISANI

Mamake mzazi nyota wa Bongo Zuchu ambaye pia ni mwimbaji na mtunzi wa nyimbo za Taarab Khadhija Kopa amefunguka na kusema kwamba Bintiye Zuchu hajaolewa ,na yeyote atakayejitokeza na kumlipia mahari ndiye atakayemtambua kama bwanake.

"Binti yangu hajaposwa hakuna yeyote amemlipia Mahari wengi kwenye mitandao wanasema Diamond ndio mpenzie ,mimi sijasikia kulingana na tamanduni zetu lazima jambo la mahari liwe kwa hivo yeyote atakayetaka kuwa na Zuchu amlipie mahari niko tayari kupokea kwa muda wowote ule",alisema Kadhija Kopa.

Kuligana na Khadija Kopa katika utamanduni wao jambo la mahusiano ya ndoa lazima lifanyike kwa taratibu zakimila, wapendanoa wakizingatia swala la kuwafahamisha wazazi kwa pande zote .

Kwenye Mahojiano haya na wanablogu wa mitandao mtunzi huyu wa nyimbo baada ya wanablogu kutaka kujua iwapo Diamond anayekesiwa kuwa mpenzi wa bintiye ndiye anafaa kulipa mahari alifunguka na kusema yeyote yule atakaye leta mahari ndio atamkabidhi nafasi ya ndoa na Bintiye Zuchu.

"Diamond si mchumba wake hajaleta mahari wala hajamuoa kwa hivo mtu mwingine yeyote anaweza kuleta pesa zake za mahari ,kwa maana mimi sipendi mahusiano ya nje napenda mambo ya wazi nimetoa nafasi kwa yeyote alete mahari",alisema Khadija Kopa.