"Niliacha kazi yangu kwa sababu ya mwanaume" Carrol Sonnie acheka upuuzi aliofanya juu ya mapenzi

Sonnie ameeleza kwamba alipiga hatua hiyo kutokana na mapenzi yake mazito kwa mpenziwe.

Muhtasari

•Sonnie alifichua hayo Ijumaa asubuhi alipokuwa akizungumzia picha za kumbukumbu zilizoibuka kwenye simu yake.

•Carrol Sonnie alionekana kujicheka mwenyewe kwa kuacha kazi yake kwa sababu ya mpenzi wake 

Carrol Sonnie katika studio za Radio Jambo
Carrol Sonnie katika studio za Radio Jambo
Image: RADIO JAMBO

Muigizaji Caroline Muthoni Ng’ethe almaarufu Carrol Sonnie amefunguka kuhusu kipindi aliacha kazi kwa sababu ya mwanamume katika siku za nyuma.

Mpenzi huyo wa zamani wa mchekeshaji Mulamwah alifichua hayo Ijumaa asubuhi alipokuwa akizungumzia picha za kumbukumbu zilizoibuka kwenye simu yake.

Katika ufichuzi wake, Sonnie alionekana kujicheka mwenyewe kwa kuacha kazi yake kwa sababu ya mpenzi wake wa zamani na akaeleza kwamba alipiga hatua hiyo kutokana na mapenzi.

“Uweh niko hapa google fotos inanikumbusha mambo ya kipuuzi niliyofanya kwa ajili ya mapenzi. Ghai, niliacha kazi kwa sababu ya mwanaume. Muthoni ma!” Sonnie aliandika kwenye Instagram.

Mama huyo wa binti mmoja hata hivyo hakufichua ni nani kati ya wanaume aliowahi kuwachumbia ambaye alikuwa akizungumzia. Aliendelea kuwaomba wafuasi wake pia kufunguka kuhusu baadhi ya mambo ya kipuuzi ambayo walifanya kwa sababu ya mapenzi.

Sio mengi yanajulikana kuhusu maisha ya uchumba ya muigizaji huyo mbali na uhusiano wake na mchekeshaji maarufu, David Oyando almaarufu Mulamwah.

Image: INSTAGRAM// CARROL MUTHONI

Wawili hao walichumbiana kwa takriban miaka minne na hata kupata mtoto pamoja kabla ya kutangaza kuachana kwao mwishoni mwa 2021, miezi michache tu baada ya kuzaliwa kwa binti yao.

Alipokuwa akitangaza kutengana kwao mnamo Desemba 2021, Sonnie alimshukuru mpenzi huyo wake wa  zamani kwa muda ambao walishiriki pamoja na kumtakia kila la heri katika hatua yake nyingine.

“Hii ni kuweka wazi kuwa mimi na Mulamwah hatuko pamoja tena, tumekubaliana wote wawili na tumeamua kuachana kwa sababu zinazojulikana kwetu, asanteni sana kwa upendo na support mliyotupa kwa miaka hiyo 4, mimi binafsi, sichukulii kirahisi,” Sonnie alisema mnamo 2021.

Aliongeza, "Kwa Mulamwah, asante sana kwa kuniruhusu kuwa sehemu ya maisha yako kwa miaka hiyo nashukuru sana na nitahifadhi kumbukumbu milele. Katika hatua yako inayofuata maishani, sitaki chochote ila bora zaidi. Endelea kushinda na Mungu akubariki katika kila hatua ya maisha yako. Kwa mashabiki wangu, asante kwa sapoti na upendo ambao mmekuwa mkinionyesha. Mungu awabariki kila mmoja wenu. Ninapoendelea na safari hii, mniruhusu niwe napamba simu zenu zenye maudhui ya ajabu na najua kwa hakika mtapenda😊. Kuvunjika kwa mwiko sio mwisho wa kupika ugali kwa hivyo tunasonga mbele na kuombea kesho nzuri😍 . Endeleeni kuunga mkono na kuonyesha upendo. Kazi izidii💪🏼"