Kumbe! Samidoh alimtazama Karen Nyamu akinengua kiuno na DP Rigathi Gachagua

Samidoh alikuwepo katika hafla ambapo DP Gachagua alionekana akicheza densi na Karen Nyamu.

Muhtasari

•Seneta Nyamu na DP Gachagua walionekana kuwa na furaha sana na tabasamu kubwa ziliandikwa kwenye nyuso zao walipokuwa wakicheza densi pamoja.

•Miongoni mwa picha kadhaa ambazo Nyamu alipost, wengi walionekana kuangazia zile ambazo Samidoh alionekana.

Image: FACEBOOK// KAREN NYAMU

Wikendi, picha za seneta Karen Nyamu akifurahia densi na naibu rais Rigathi Gachagua wakati wa hafla ya mahari ya Mbunge wa Mathira Eric Wamumbi na Mwakilishi wa Wanawake wa Murang’a, Bi Betty Maina zilisambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii.

Wanamitandao wa Kenya walitoa maoni mseto kuhusiana na picha hizo, baadhi wakifanya utani huku wengine wakiunda memes za kuchekesha kutokana nazo.

Karen Nyamu alikuwa wa kwanza kuposti picha hizo kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii Jumamosi jioni na alionekana kufurahia kujiburudisha na naibu rais.

"Meri na kuna!" alisema kwenye picha alizochapisha kwenye Facebook.

Kumaanisha: “Hatua mbili na kupinda” ambayo ni densi ya Wakikuyu.

Katika picha hizo, wanasiasa hao wawili walionekana kuwa na furaha sana na tabasamu kubwa liliandikwa kwenye nyuso zao walipokuwa wakicheza pamoja.

Siku ya Jumapili, seneta Nyamu alishiriki picha zaidi za hafla ya mahari ya Jumamosi ambapo alionekana akitangamana na wageni wengine. Miongoni mwa picha hizo ni zilizomuonyesha akiwa na mpenzi wake Samuel Muchoki almaarufu Samidoh ambaye ni wazi pia alikuwepo katika hafla hiyo.

Miongoni mwa picha kadhaa ambazo Nyamu alichapisha, wanamitandao wengi walionekana kuangazia zile ambazo mwimbaji huyo wa Mugithi alionekana.

Tazama maoni ya baadhi ya wanamitandao;-

Triza Wainaina: Hakuna ila mapenzi. Wanandoa wazuri. Samidoh wetu na kufurahi nayo, ni amani.

Wanguii Wa Rware: Jamaa huyu alipata amani.

Shiku Mkono: Mscorpio Mlookalike mnakaa fitii, ruracio yenu ndio inayofuata.

Esther Mwangi: Hata uumpost, ujue ni wa wenyewe ulijinyakulia.

Vickline Omoigwa bwa’Abagesaka: Upendo unashinda, na mnafanana sawa.

Katika mahojiano ya hivi majuzi, seneta Nyamu alibainisha kuwa DP Gachagua alikuwa sahihi kumsuta hadharani mpenzi wake Samidoh mapema mwaka huu.

Mwezi Januari mwaka huu, naibu rais alipokuwa akitoa hotuba yake katika hafla, alimtaka staa huyo wa Mugithi kuchukua udhibiti kamili wa mahusiano yake kufuatia tukio baya lililotokea jijini Dubai mwishoni mwa mwaka jana ambalo lilimhusisha yeye, mke wake wa kwanza Edday Nderitu na Karen Nyamu.

Katika kauli yake, DP Gachagua alisema kuwa mwanamuziki huyo amepata heshima ya wengi kupitia tungo zake za muziki na ni wakati wake sasa kurejesha utulivu katika familia yake na kuhakikisha adabu inatawala.

"Sasa wewe Samidoh ucontrol watu wako. Panga panga hiyo maneno yako na ukishindwa, tutakukataza kwenda kwenye wimbo," Gachagua alimwambia Samidoh kwa utani wakati wa ibada ya mazishi ya dadake waziri Moses Kuria, Pauline Nyokabi.

Katika mahojiano ya hivi majuzi kwenye chaneli ya YouTube ya Convo, seneta Karen Nyamu alimtetea naibu rais akisema kuwa alikuwa sahihi kumtaka mzazi mwenzake kudhibiti nyumba yake.

Mama huyo wa watoto watatu alikubali kwamba tukio la kusikitisha lililotokea jijini Dubai lilikuwa kuteleza kwa upande wa Samidoh.

“Si mzaha. Hali kama ile iliyotokea Dubai haikuwa ya mzaha, ilikuwa mbaya na ilikuwa kuteleza kwa sehemu yake (ya Samidoh)," Karen Nyamu alisema.

Aliongeza, "DP alikuwa akimsuta kwa sababu ilikuwa ni upotovu kwa upande wake kabisa."