Jamaa ahama plot kisa watoto majirani kutaka awafanyia homework ya hisabati na fizikia

Kilichomuudhi Zaidi ni kwamba watoto hao walikuwa wanamuona msomi sana na mwenye maarifa katika masomo mawili tu – fizikia na hesabu.

Muhtasari

• “Hilo ni jambo zuri na lenye afya ambalo watoto hao wanafanya. Ina maana wanakuheshimu na kukuamini na kukuona kama mshauri ❤️” mwingine alimwambia.

Hisabati
Hisabati
Image: BBC NEWS

Mwanamume mmoja amezua mjadala mkali mitandaoni kwa kufichua sababu ya msingi ambayo ilisababisha wakati mmoja akahama katika nyumba za kupangisha ambazo alikuwa anaishi mjini.

Jamaa huyo kupitia mtandao wa X, awali ukijulikana kama Twitter aliandika kwamba alikuwa amepangisha nyumba ya makazi katika mtaa mmoja mzuri lakini kulikuwa na kero moja ndani ya zile nyumba.

Alisema kwamba alikuwa anataabishwa na kukoseshwa Amani na watoto wa majirani zake ambao walikuwa kila mara wanatoka shuleni jioni na kujitoma ndani mwake wakimtaka kuwapa msaada wa kufanya kazi za ziada ambazo wamekabidhiwa na walimu wao kutoka shuleni.

Kilichomuudhi Zaidi ni kwamba watoto hao walikuwa wanamuona msomi sana na mwenye maarifa katika masomo mawili tu – fizikia na hesabu – na hizo ndizo kazi za ziada ambazo kila mara walikuwa wanakuja kwake wakimtaka kuwasaidia kutatua.

Kauli yake: "Sababu moja kuu iliyonifanya kuacha nyumba yangu ya zamani ni kwa sababu watoto wa jirani yangu kila wakati huleta kazi zao za nyumbani za hesabu na fizikia kwa sababu walisikia nilisoma fizikia."

Alidai kuwa hiyo ndiyo sababu kuu iliyomfanya aondoke, kwani kila mara walikuwa wakimsogelea kutokana na historia yake ya masomo ya fizikia kutoka chuo kikuu.

Hata hivyo, baadhi walimlaumu kwa kutotaka kutoa mchango katika jamii kwa kuwasaidia watoto huku wengine wakimtetea kwamba kazi za ziada si za kusaidiwa kufanywa na mtu mwingine.

“Oga ni nini mchango wako kwa jamii kama mhitimu wa Fizikia? Je! sivyo unavyopaswa kufanya?” mmoja alimuuliza.

“Hilo ni jambo zuri na lenye afya ambalo watoto hao wanafanya. Ina maana wanakuheshimu na kukuamini na kukuona kama mshauri ❤️” mwingine alimwambia.