Matokeo ya KCPE kutangazwa wiki hii, Usahihishaji wa KCSE wang'oa nanga

Muhtasari

•Haya yanajiri huku usahihishaji wa mitihani ya KCSE ukielekea kuanza kote nchini. Mtihani huo unaingia wiki ya tatu na ya mwisho.

•Mwaka huu KNEC ilisajili watahiniwa 1,225,507 katika vituo 28,316 vya mtihani wa KCPE ikilinganishwa na watahiniwa 1,191,752 katika vituo 28,467 mwaka wa 2020.

Watahiniwa wa darasa la nane wakalia mtihani wa KCPE
Watahiniwa wa darasa la nane wakalia mtihani wa KCPE
Image: MAKTABA

Hatima ya watahiniwa milioni 1.2 waliofanya mtihani wao wa KCPE 2021 hivi majuzi itajulikana  Jumatatu au Jumanne.

 

Haya yanajiri huku usahihishaji wa mitihani ya KCSE ukianza kote nchini. Mtihani huo unaingia wiki ya tatu na ya mwisho.

 

Walimu ambao watakuwa wakisahihisha Kiingereza na Hisabati wataripoti katika vituo vya usahihishaji vilivyoteuliwa siku ya Jumatatu.

Mitihani ya KCSE itasahihishwa katika maeneo tofauti kulingana na aina ya karatasi.

"English Pp 3 itasahihishiwa Alliance High na Thogoto TTC, Maths Pp 2 itasahihishwa katika shule ya Lenana," mwalimu ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema.

Karatasi ya Kiswahili Pp 1 na Karatasi ya Historia Pp1  zitasahihishiwa Alliance Girls na Starehe Boys mtawalia.

Mwalimu mwingine alisema watasahihisha Jiografia Ppn1 na Karatasi na Biolojia Pp2 katika Muranga TTC na Limuru Girls kwa utaratibu huo.

Wasaidizi wa watahini wakuu wa masomo hayo mawili, Kiingereza na Hisabati, walianza kuripoti katika maeneo yao mahususi siku ya Ijumaa.

Walimu watakaoshiriki katika usahihishaji wa KCSE 2021 watatarajiwa kuripoti katika shule za Moi Forces Academy, Sunshine High, State House Girls, St Georges na Upper hill.

Vituo vingine vya usahihishaji ni Loreto Girls Limuru, Langata High,Kenya High, Thika High, Buruburu High na Moi Girls Isinya.

Kufikia Ijumaa wiki jana, watahiniwa kadhaa walikuwa wamemaliza mitihani yao na kuenda nyumbani.

Wanafunzi wasiofanya masomo ya Fizikia, Biashara, Kilimo na Jiografia hawatakuwa na mitihani yoyote wiki hii.

Kuanzia Jumatatu, watahiniwa waliosalia shuleni watakuwa na Karatasi ya Fizikia Pp1 na Jiografia Pp 1 siku ya Jumatatu, Karatasi ya Biashara Pp1  na Karatasi ya Jiografia Pp1 zitafanywa Jumanne.

Karatasi za pili za Fizikia na Jiografia zitafanywa Jumatano, Biashara na Kilimo (Karatasi ya 2) zitafanyika Alhamisi.

Siku ya mwisho itakuwa Ijumaa ambapo wanafunzi wafanya Physics Practicals.

Mwaka huu KNEC ilisajili watahiniwa 1,225,507 katika vituo 28,316 vya mtihani wa KCPE ikilinganishwa na watahiniwa 1,191,752 katika vituo 28,467 mwaka wa 2020.

Hili linaonyesha ongezeko la 33,755 sawa na asilimia 2.75.

(Utafsiri: Samuel Maina)